MAHITAJI

Magimbi/majimbi nusu kg
Nyama (yoyote) nusu kg
Tomato fresh 1
Kitunguu maji 1
Kitunguu saum 1 tsp
Tangawizi mbichi 1 tsp
Chumvi kiasi
Pilipili ya kuwasha (ukipenda)
Bizari ya mchuzi (ukipenda)
Tui zito kikombe 1 mpaka 1 na nusu

NAMNA YA KUPIKA

13418898_500122566863366_9060231723325302610_n
Ipike nyama pamoja na chumvi, kitunguu saum na tangawizi, tia maji ya kiasi mpaka inawiva ibaki na supu kiasi ,
Menya magimbi yakate kate kiasi yakoshe na yachemshe pembeni kwa dakika 5 yalainike kidogo tu yamwage maji yachanganye pamoja na nyama uliyoichemsha,
Kata kata tomato na kitunguu maji ukipenda visage, tia kwenye sufuria ya magimbi, pamoja na pilipili na bizari ya mchuzi , funika wacha vichemkie supu karibu na kukauka tia tui , funika wacha vichemke na tui mpaka vibaki na rojo kiasi unavyopenda , epua na ENJOY. *ukipenda unaweza kutia bizari nyembamba/uzile na pilipili manga
*sio lazima kuvichemsha ila ni vizuri kuvitoa utomvu.