KAIMATI ZA MAZIWA YA UNGA
Unga ngano vikombe 2
Maziwa ya unga kikombe 1
Sukari 1 tbsp
Hamira 1 tbsp
Mafuta ya uvuguvugu 2 tbsp
Maji ya uvuguvugu kikombe 1 na nusu mpaka viwili kasrobo
Mafuta ya kuchomea

kaimati-picture-courtesy-of-kenyafood-wordpress-com

Tia kila kitu kwenye bakuli changanya vizuri upige kwa mkono kwa dakika 2 hadi 3 kisha uweke sehem uumuke,
Zikiumuka, teleka mafuta yapate moto, chota mchanganyiko kwa kutumia mkono au kijiko kiasi uchome kwa moto wa kiasi zigeuze ziwive vizuri pande zote zitoe ziweke pahala zijichuje mafuta, wacha zipoe
SHIRA
Sukari kikombe 1 na nusu
Maji kikombe 1 na nusu
Iliki ya unga au vanilla essese/arki ya vanilla 1 tbsp

Weka kwenye sufuria vitu vyote ivyo vya shira ipike mpaka ianze kua nzito kiasi (isianze kuganda) iwe nzito kiasi tu iepue ,kaimati zikishapowa zitoe kwenye shira zigaragize vizuri , zitoe ziweke kwenye chombo na ENJOY.

Comments

comments