Wengi wetu huwa tuna dhani kuweka dawa na kufanyia steaming ndio kutakuza na kufanya nywele zetu kuwa na afya, hivyo utakuta mtu ana weka dawa kila baada ya mwezi na kufanyia steaming kila baada ya week mbili. Hii ndio husababisha nywele kunyonyoka na kutokua na afya.
Dawa si nzuri sana kwa nywele zako hivyo una shauriwa kuweka dawa mara mbili au tatu kwa mwaka. Hii ina maana uweke dawa kila baada ya miezi sita hadi minne. Lakini swali linakuja je katika kipindi hiko chote ambacho nywele zina oteana na kukua uta fanyaje hili zisikatike? hizi ndizo tips muhimu za nini ufanye
1) Deep Condition – fanyia deep condition mara kwa mara hii itasaidia kurainisha nywele zako na kuipa nywele afya, wakati una fanyia deep condition ni vizuri ukaosha nywele na maji ya baridi na pia usikae kwenye moto, paka condition yako funga mfuko wa plastic na taulo juu kaa nalo kwa nusu saa osha.
2)paka mafuta ya nywele kila siku – hii ni muhimu mno kwa nywele zako uli kuzipa nywele unyevu na kurainisha ili kuzuia ukatikaji wa nywele ni muhimu uwe una paka mafuta mara kwa mara, na mafuta mazuri kwa ajili ya nywele ni mafuta ya kumiminika na si mafuta ya mgando. Eg olive oil ya maji au mafuta ya nazi ya maji.
3) Kata ncha- Kukata ncha kunasaidia ukuaji wa nywele pia husaidia kujaza nywele.
4) Suka misuko ambayo haikati nywele – ipo mingi sana una weza ku google “protective hair styles” ukaipata lakini pia nywele za kurudi nyuma “twende kilioni” husaidia mno ndio maana utakuta wanafunzi wengi wana nywele ndefu zilizo na afya.
5)Punguza kukaa/kutumia vitu vya moto – kutumia pasi au dryer kukaushia au kunyooshea nywele mara kwa mara kuna athiri nywele, nywele hupoteza ubora wake kutokana na moto. Hii huathiri hata zile nywele zinazo ota. Kama una osha nywele mara kwa mara ni vyema ukaziacha zikauke zenyewe na upepo.
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…