Kupunguza kitambi/tumbo ni changamoto kubwa ni kitu ambacho kina tunyima amani wengi lakini namna ya kukipunguza huwa ni ngumu sana, wengi huwa tuna fanya diet au kuamua kwenda gym kweli zina weza kusaidia lakini kama huwezi hivyo vyote ni nini ufanye?

  1. Kunywa maji – mara nyingi huwa tunakua wavivu kunywa maji, lakini ukijiwekea kuwa una kunywa maji mengi/mara kwa mara kwa siku itakusaidia kuto kusikia njaa, hii itakufanya uwe mbali na vyakula vyakula vya hapa na pale visivyo kuwa na msingi lakini pia maji yana saidia kufanya ngozi iwe nyororo so ni maji maji maji maji. unaweza kuongezea vitu kama limao, tango, tangawizi katika maji yako inaitwa detox water ingia hapa kusoma zaidi

2.Pata Usingizi wa kutosha – hii itakuepusha na kutaka kula chakula usiku sana, unapo wahi kulala unawahi kula hii inasaidia mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizuri.

3.Punguza/Acha Kunywa Soda – Sukari ni moja ya vitu vibaya vinavyo anzisha/kuleta unene kaa mbali nazo na anza kunywa maji kwa wingi, kuna vitu vingi ambavyo husabisha tumbo lisipungue kuvijua zaidi soma hapa

4.Weka Ratiba Ya Chakula – ni vizuri kama utakuwa unajipikia mwenyewe maana utajua uweke chumvi, sukari kiasi gani, mafuta nk. Pangilia ratiba yako ya week nzima lakini pia katika ratiba yako weka healthy food ambazo zitakufanya uweze kupuguza mafuta mwilini, unaweza kusoma hapa kupata idea ya nini unatakiwa ule

5.Acha Kula Vitaunwa Vidogo Dogo – biscuits, Big G, Chocolate ni vitamu na vina temptation sana lakini navyo vinaongeza sukari na kusababisha kuleta unene tumboni jaribu kuviepuka sana tembea na fresh juice, unapo jisikia kula kitu kitamu kitamu kunywa juice.

6.Kula taratibu – yes hili huwa tunalishindwa sana, lakini kula taratibu kuna saidia kumeng’enya chakula chako vizuri lakini pia kunafanya ule chakula kidogo na kushiba haraka.

7.Mafuta si rafiki yako – mafuta ni mabya sana katika chakula jaribu kutumia mafuta yenye less cholesterol, kama mafuta ya nazi, olive oil, almond au pika chukuchuku ukiongezea chakula chako na parachichi, parachichi linaweza kusababisha chakula kiwe kitamu na lina mafuta ambayo hayana madhara

Njia 7 Za Kupunguza Kitambi Haraka

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com