Aliyekuwa mshindi wa Miss Talent (Muttichoice)katika shindano la miss Tanzania 2010 Flora Florece, ambaye sasa amekuwa kaijishughulisha na biashara za binafsi katika mji wa Morogoro.

10980705_1455790644676351_8447077578459602718_n

Licha ya baishara zake lakini pia Flora amekuwa mdau wa mashindano mbalimbali ya urembo katika Mji wa Morogoro na kwingineko.

Flora hakusita kuweka wazi kile kinachoonekana kuzorotesha tasnia ya urembo katika mji wake wa Morogoro, ambapo aliliambia jarida la Mweeh “Kuridhika na mataji ya hapa mkoani ndio kinachofanya washindwe kufanya vizuri ngazi ya taifa,kiukweli hawafanyi bidii wakifika katika mapambano yale makubwa. Licha ya mimi kuwapa moyo na hata  kuwapa mbinu za kupambana bila kukataa tama ili kuhakikisha ushindi unapatikana, lakini hata hivyo bado imekuwa tatizo sugu.