Miss Tanzania 2015 Lilian Kamazima ameanza maandalizi yake ya kujiandaa kuelekea Sanya nchini China kwa ajili ya shindano la Miss World.Lilian akiwa ni miongoni mwa wasichana 120 ataiwakilisha Tanzania katika shindano hilo, Lilian ameonekana akiwa na watu mbali mbali ambao wana husiana na mitindo akiwemo kiki fashion pia miss Tanzania mwaka jana Hapiness  Watimanywa akipewa ushauri au njia za kumfanikisha kushinda katika shindano hilo.

happy

Lilian akipewa mawili matatu na alie kuwa Miss Tanzania 2014 Hapiness

Ratiba yenyewe iko hivi, mrembo wetu Lilian pamoja na warembo wengine wote watapokelewa China November 21 2015 kwenye moja ya Hoteli kubwa iliyopo Sanya na kambi yao itakuwa hapo kwa muda wote mpaka siku ya fainali December 19 2015.

unnamed

Lilian akiwa na Kiki

Kingine tunachotakiwa kukifanya ni kumpa support ya nguvu mrembo wetu Lilian Kamazima kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo hiyo njia pia itamfanya asogee kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi wa Miss World 2015.

 

LILIAN KAMAZIMA NA MAANDALIZI KUELEKEA MISS WORLD 2015

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com