tangazo

Tangazo batili linalo kataza baadhi ya mavazi

wizaraWebsite ya ukweli ya wizara ya utamaduni,sanaa na michezo

Takribani siku mbili zilizopita zilienea taarifa juu ya katazo rasmi la mavazi ya nguo fupi,surualina mavazi ya kubana  ambalo ilisemekana limetolewa na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Akiongea na Power Breakfast asubuhi ya leo, waziri mwenye dhamana ya Wizara hiyo, Mh Nape Nnauye amekanusha juu ya taarifa hiyo:
“Taarifa hizo si za ukweli, nasikitika sana watu wanatuma taarifa hiyo kwenye mitandao tofauti ya kijamii, Wizara imesikitika kwa kusambazwa kwa Taarifa hiyo ikianisha picha ya mavazi ambayo yamepigwa marufuku, naomba chombo kinachohusika kichukue hatua dhidi ya watu waliohusika na taarifa hiyo potofu ili watu wengine wajue sheria inafuata mkondo wake.” Mh. Nape Nnauye

Comments

comments