Tumekuwa tukiona Wabunifu mbalimbali kutoka Nchi za wenzetu wakiwa wanabuni haya mavazi yaliyopewa jina la Tulle, kwetu hakukuwa na designs za aina hii nyingi. Mara nyingi tulikuwa tukiziona kwa mbunifu Jacqueline Wolper lakini week hii tumeona wabunifu wengine wawili wakitoa mavazi ya aina hii.

Ambao ilitufanya tufikiri may be ndio trend mpya tuitegemee au wabunifu wetu wameamua kutoka Nje ya box walilojiwekea. Oh well hatusemi hiki ni kitu kipya maana tumesha kiona katika runways za wabunifu mbalimbali kama Giambattista Valli’s, Molly Goddard , Off White na wengine wengi. Lakini tunapenda haya mabadiliko ya ladha tunayoyaona tulilalamikia nguva siku hizi zimepungua, tumeona column dress na sasa tupo kwenye Tulle style.

Taratibu tunaanza kufanya mabadiliko ya maana ambayo tunadhani mwishoni yatatufanya tuache sasa kuangalia wenzetu na kuanza kutengeneza vya kwetu.

Week hii tumemuona mbunifu Eve Collection ambae yeye alimvalisha Mama Diamond katika birthday yake, ambapo alimvalisha layered tulle red dress, ambayo ilikuwa na turtle neck na long sleeves.

Pia tumemuona mbunifu Jacqueline Wolper yeye akiwa amevalia her own creation, amevaa high low black tulle dress

Wakati mfanya biashara j_adoreintz, ambae yeye alikuwa sponsor wa miss Mwanza 2019, aliattend event hio akiwa amevalia red tulle dress kutoka kwa mbunifu Johnny Jephy

Well we are so glad kuona ubunifu ukibadilika badilika lakini tuambie kwako unaionaje design hii ya mavazi?