SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mbunifu Asya Khamsin Na Maoni Yake Kuhusu Tanzania Red Ribbon Gala
Mitindo

Mbunifu Asya Khamsin Na Maoni Yake Kuhusu Tanzania Red Ribbon Gala 

Ikiwa tunaelekea katika kilele cha Tanzania Red Ribbon Gala, tumewatafuta baadhi ya wabunifu watakao shiriki katika Tamasha hili na kuwauliza maswali mawili matatu kuhusu Tamasha hilo.

Hapa tupo na mbunifu Asya Khamsin ambae amejibu maswali yetu kama ifuatavyo

AFS: umeona umuhimu gani wewe  au company  kuungana na campaign ya fashion fighting AIDS

Asya: Mimi kama Malkia wa nguvu 2019 katika fashion and beauty tanzania nina umuhimu sana kushiriki katika red ribbon 2019 event Kwani ni event ambayo inabeba ujumbe mkubwa ka toka jamii haswa kwa kupiga vita Na kujiepusha Na maradhi ya ukimwi Kwani ni ugonjwa uliopukutisha vijana wengi kwa ujumla so ushirikiano wangu Una umuhimu sana kwa kufikisha ujumbe wa kuzidi kutumia Kianga Na kujiepusha Na ugonjwa huu.


AFS: Ikiwa Red Ribbon Gala ni event ya fashion na ina purpose kubwa nyuma yake, Je Tutegemee collection hii itawezaje kuhamasisha jamii kutokana na ugonjwa wa Ukimwi?

Asya: Collection yangu itakuwa Na rangi 2 kama ilivyo kawaida rangi nyeusi Na nyekundu Na pia kutakuwa Na mapambo ya condom ambayo huo ni ujumbe tosha wa kuhamasisha kutumia kinga kwa ajili ya kuepukana Na ugonjwa wa ukimwi.


AFS: Je unatumiaje ubunifu wako kusaidia jamii inayo kuzunguka?

Asya: Nimetumia Na bado naendelea kutumia ubunifu wangu kwa kusaidia jamii inayonizunguka. Nipo katika fashion industry kwa miaka 40 Sasa nilikuwa naandaa majukwaa makubwa 2 (lady in red Na Kanga Za kale) Na nilikuwa Nakaribisha wabunifu chipukizi wengi sana kuweza kuonyesha vipaji vyao Na Sasa wamekuwa ma Star wakubwa tu Na pia wabunifu pamoja na models wengi tu mpaka sasa wanahitaji msaada wangu Nami nawatumikia vilivyo mpaka wanafikia malengo naweza kusema mimi ndie nilipe anzisha kupanda ka wabunifu zaidi ya mmoja tanzania Na wengine wakafuata nyayo Na ndio maana nikapata award ya lifetime achievement award Na humanitarian award Na kwa Sasa tuna Chama cha designers FASHION ASSOCIATION OF TANZANIA NIKIWA VICE PRESIDENT WAKE

Related posts