Wabunifu wanazidi kujaribu kuleta mambo tofauti na kuwa creative katika runways zao, tuliona jinsi Gucci alivyo amua kugeuza runway yake kuwa operation room kwa kuwabesha models vichwa fake vilivyo fanana nao, Mbunifu Moschino nae aliwapaka rangi models wake na kuwa kama cartoons au aliens lakini mbunifu huyu kutoka China yeye ameamua kuwavalisha models wa kiume mimba fake.

Katika London Fashion Week Men’s collection ya mbunifu wa ki-Chinese  Xander Zhou wanamitindo wake walipanda jukwaani wakiwa wamewekwa mimba fake,

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mbunifu huyo alipost picha ya model ambae amevalia T-shirt iliyo andikwa New World Baby na ku-caption “At Supernatural, Extraterrestrial & Co., we’re prepared to welcome a future of male pregnancy.”

Wengi wamekuwa wakisema kwamba nia ya mbunifu huyu ni kuleta awareness katika haki sawa kati ya wanaume na wanawake hata katika kubeba mimba

Wakati wengine wakisema hii sio fashion wala sio art ni upuuzi,

Inaweza ikawa sio fashion wala art lakini onething is for sure ni kwamba Xander Zhou ame trend sana kutokana na hii idea na hata wale ambao walikuwa hawamjui sasa wanamjua

well tupe maoni yako je kwako wewe unaona hii imekaaje?

Comments

comments