Ni vigumu kuwa ume msahau, Miriam Odemba ni jina ambalo lime vuma sana mnamo mwaka 2008-2010, ni miss Tanzania earth 2008 ambae ametuletea mataji mengi mno nyumbani. Odemba ambae kwa sasa anaishi nje ya nchi pamoja na familia yake huku akiendelea na kazi zake za mitindo. Hivi karibuni alienda Paris katika Paris Fashion Week na kama ambavyo wanasema mwenye asili haachi asili au mkataa kwao mtumwa Miriam Odemba ambae amezaliwa Arusha Tanzania ameonekana akiwa Paris huku amevalia kiremba cha shuka la kimasai.

 

 

2

 

6 4 5 7