Fanny Packs zimekuwa kwenye trend kwa muda sasa ni vijipochi fulani vya kuvaa kiunoni, watu maarufu mbalimbali wameonekana wakiitumia trend hii, fashionista’s, stylist na wengine wengi. Lakini pia designers wakubwa kama gucci wameonekana kubuni vipochi hivi katika collection zao, hapa kwetu wasanii kama Dogo Janja,Juma Jux wameonekana kuvutiwa na trend hii pia.

Tunajua kwa sasa tuna Hijabista’s mbalimbali ambao wanatuonyesha namna ya kuwa modest huku ukiwa umejistiri na leo tumekuletea namna ambavyo hijabista mbali mbali wame jaribu kustyle trend hii huku wakiwa wamejistiri.

Hijabista Fatema yeye ameonyesha namna ya kustyle fanny pack na pleated skirt na turtle neck top, amemalizia muonekano wake na boots.

Wearing one color is so in right now hijabista huyu yeye amevaa wide leg pants za red, top ya red na funny pack ya rangi hio hio huku akimalizia muonekano wake na brown sandals na brown hijab.

Hijabista Mariam Mohammad yeye amevaa fanny pack yake nyeusi na long tuxedo dress/coat nyeusi na ruffle blouse nyeupe huku akimalizia muonekano wake na hijab nyeupe na long black heels.

Mariam tena akiwa amebeba fanny pack yake nyeusi huku akiwa amevalia all white assemble lakini mtoko huu ni casual zaidi.

Tuambie wewe ungestyle vipi fanny pack yako?

Comments

comments