SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Pata Kujua Kuhusu Layering Na Inavyoboresha Uvaaji
Mitindo

Pata Kujua Kuhusu Layering Na Inavyoboresha Uvaaji 

Nitatumia zaidi neno ‘kulayer’ kwasababu ni fupi zaidi kuliko kutumia sentensi ‘kuvaa nguo juu ya nguo’ ila nachomaanisha ni kitu kile kile. Kulayer hufanya hata nguo ya kawaida kabisa kuwa na muonekano wa kipekee na tofauti. Ni namna ya kuongeza ubunifu na upekee katika vazi. Unaweza kufananisha kulayer na icing sugar na urembo juu ya cake, cake inaweza kuwa ile ile ndani ila unavyoweka icing, rangi na maua yake yanafanya cake ile kupata muonekano fulani. Inasaidia upate looks/ mionekano mingi tofauti kwenye vazi moja. Kuliko kununua nguo nyingi sana ni muhimu kujua nguo inahitaji kufanyiwa layer kwa namna gani ili niweze kuivaa kwa namna nyingi tofauti. Kulayer kuna hatua au sehemu zake. Katika kulayer kuna mavazi aina tatu yanayohusishwa yani kulayer ni muunganiko wa Vazi la msingi/ muhimu (basic) + vazi la kunogesha (complimentary) +Nakshi (accessories). Inawezekana hujanielewa bado hivyo haya hapa maelezo kuhusu hayo mavazi;

Nguo ya msingi (Basic)

Unapovaa nguo kabla haujaongeza mbwembwe yoyote ile sio koti wala si urembo wala kimono hii/hizi ndio nguo msingi. Yani kile unachovaa tu kufunika mwili. Kwa mfano jeans na vest. Hili ni vazi plain tu.

Nguo ya kunogesha(Complimentary)

Hii/hizi nguo ni kiungo sasa,mbwembwe au maonjo. Inalipa vazi la msingi utofauti. Ni nguo unayoongeza juu ya nguo ya msingi. Inaweza kuwa koti, kimono, jacket,scarf, vest,vest coat,n.k. Inaweza kuwa haya ni sketi juu ya suruali, vest juu ya shati la mikono mirefu. Kiujumla ni nguo unazoweka juu ya nguo nyingine. Hizi nguo zinafanya vazi lako liendani na mandhari fulani au lifae kwa ajili ya tukio fulani.

Nakshi (Accessories)

Hivi ni vitu vyote vinavyoongezea nguo zako umaridadi. Naongelea cheni,kofia,mkoba,pete,hereni n.k. Nadhani umenisoma. Nakshi hufanya uonekane umepangiloa mavazi yako zaidi.

Hii mifano ni kukusaidia uelewe zaidi kuhusu kulayer.

Hapa nguo basic ni vest na jeans na namna nne unazoweza kulayer. Unaweza kulayer kwa njia nyingi zaidi. So badala ya kununua jeans pair tano na top tano unaweza kununua jeans na top moja kisha ukanunua mavazi kadhaa ya kunogesha. Kwa nguo ile ile unaweza kupata looks nyingi sana. Na ukinunua nguo ukiwa na hili wazo kichwani itakuwa ngumu kwako hata kuwa na nguo ambayo haina kitu cha kuvalia

Hapa nguo basic ni Shirt dress ambayo pia ina njia tofauti za kulayer. Nguo basic au ile nguo ya msingi unaweza ivaa kama ilivyo pia. Hapa shirtdress imefanyiwa ‘layering’ kwa nakshi tu, kwa suruali (yes kulayer sio lazima uweke kitu juu hadi kwa chini au ndani ni kulayer),kwa sketi na pia koti.

Katika kipindi cha baridi pia unaweza kuuboresha muonekano wako na kuongeza joto kupitia nguo kwa kuvaa nguo au nguo kadhaa juu ya nguo.

Hayo ndio machache kuhusu kulayer. Tumia njia hii kubadili au kuboresha muonekano wako.

Related posts