Tumezoea kuona accessories zinazotrend kama viatu, mikufu, handbags, mikanda etc ni mara chache kukuta scarf ipo kwenye trend lakini kwa sasa scarf imechukua nafasi kubwa kwa pande zote mbili kwa wanawake na wanaume.

Kwa upande wa wanaume tumewaona wakiitumia kufunga shingoni kama tai, watu maarufu mbalimbali ambao tumewaona kwenye style hii ni kama mwanamuziki Whozu, Na watangazaji Perfect Crispin Na B Dozen, wakiwa wamevalia t-shirts ama shirts. Kwetu tunaona ni accessory nzuri katika kuongezea chachu kwenye muonekano wako lakini pia unahitaji kuwa muangalifu kwenye kuchagua rangi gani uvae na mavazi yapi na sehemu unayoenda, definitely huwezi kuvaa mtindo huu wa scarf ofisini.

Whozu
Bdozen & Perfect Crispin