Ramadhani inaendelea na kumi la kwanza linakaribia kuisha, katika pita pita zetu tumekutana na fashionista’s wawili ambao outfit zao zimetuvutia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani

Kama ambavyo tulisema uhitaji kutumia au kununua mavazi mapya mwezi huu unaweza kutumia yale uliyonayo ndani na kuyageuza yakakaa modest

well tuanze na Mwamvita ambae yeye alivaa two pieces kitenge outfit, ambapo alivalia na socks & heel trend amemalizia muonekano wake kwa kuning’iniza kitembaa mabegani na amefunga turban yake vizuri kabisa. Well to us huu mtoko ni classy & trendy unaweza kuvaa kazini, meetings na hata ukialikwa ftari.

Wa pili yeye ni Penniel Mngazija yeye alivaa bandage dress nyeusi ambapo alimalizia muonekano wake na blue M2 MALLETIER Bag, Denim coat ambalo alining’iniza mkononi off white & pink sneakers akamalizia na miwani na pink lipstick na some jewelries, huu mtoko ni wa casual una weza kuvaa katika matembezi kama shopping au ukiwa una meet na marafiki.

 

well tuambie wewe ni yupi kati ya hawa wawili leo Mwamvita au Peniel?

Comments

comments