Hivi ni vigezo gani vimetumika kwa Lemutuz kuwa official Judge wa Miss Morogoro 2018?  Tuseme tu sio morogoro bali mkoa wowote ule, Lemutuz anawezaje kuwa judge na kuchagua Miss anaefaa? Kuna vitu vinachekesha kuchekesha katika uhalisi wa mambo jinsi sasa ambavyo Miss Tanzania inaendelea kufanyia katika ngazi ya Mikoa.

Moja ya shangazo kuu ni Lemutuz kuwa official Judge wa Miss Morogoro, hivi wametumia vigezo gani kumpa?. Au wametazama kwa kuwa huwa anapost wabebez basi wakaona anafaa kabisa kuwa Judge katika mashindano hayo? (Aibu).Kwanini wasitumie watu wenye ujuzi na mambo hayo? kwa maana ya mamiss ambao walishapita katika uwanja huo? Mfano Morogoro yupo Flora Florence ambaye aliwahi shinda kitaifa Multichoice Miss Talent 2010, kwanini wasimtumie mtu kama huyo kiasi wamtumie Lemutuz?

Kama kweli tunataka tuendelee ni vyema kutumia watu wenye ujuzi, ubabaishaji katika swala zima la urembo halitaweza kutusaidia bali kuzidi kuua tasnia kwa ujumla. Tunalia kila siku serikali iangalie na uwanja wa urembo pia wakati sisi wenyewe ndio tuna yashusha hadhi haya mashindano, Inakuwaje umuweke mtu ambae hata hajui kinacho endelea na kuwaacha wajuao? Je unadhani utapata chaguo sahihi la watu kufurahia mpaka serikali ikaamua kusaidia? Tulitegemea kuona former miss, au watu wanaohusiana kiundani katika mitindo, Hakika mkistaajabu ya Rukwa mtayaona ya Morogoro ya Lemutuz kuwa Official Judge.

Sisi tunaendelea kutafakari ni vigezo gani vimetuka kwa Lemutuz kuwa Official Judge wa Miss Morogoro 2018, kiasi cha kuachwa kwa watu wenye ujuzi katika mji huo?

Ukistaajabu Ya Miss Rukwa Utayaona Ya Lemutuz Kuwa Official Judge Miss Morogoro

Comments

comments


Post navigation


Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com