Jumatano ni siku ambayo sisi tuaiita wedding Wednesday, hapa huwa tunaongelea swala zima la mitindo ya harusi iwe bride maids, maharusi, reception chochote ambacho kinahusiana na mitindo ya harusi utakipata hapa. Leo tunaongelea Wedding pants hizi ni yale mavazi ya harusi yaliyobuniwa ila kwa style ya suruali. Mara nyingi wanaume ndio huvaa suruali katika harusi wanawake wao huwa wanapenda ku-stick na magauni yao.

Sisi tunasema jaribu kuwa tofauti for a change, tunajua huwezi kuingia nayo kanisani au msikitini ukafungishwa ndoa nayo lakini unaweza kuvaa kama reception dress au kama una wasimamizi ( bride maids) ambao wangependa kuonekana tofauti basi unaweza kuwavalisha hili vazi.

Suruali zipo comfortable na zinaonyesha umbo lako vizuri, unaweza kuvaa hata kwenye bridal shower

Lakini pia unaweza kuvaa kama mgeni mualikwa wakati mwingine ungependa kucheza na kutembea bila ya kushikilia gauni basi ukiwa na mood hii mplekee tu fundi akushonee elegant pants na top kali kwelikweli kwa ajili ya harusi.

 

katika majukwaa ya matindo mwaka huu wedding pants zimeonekana ku- trend sana katika collection za wabunif mbalimbali kama hizi ambazo tumetoa katika collection za wabunifu tofauti katika Lagos Bridal Fashion Week 2018

Unaweza kuvaa kama jumpsuit pia,

Tuambie kwako ni yay or nay?

Wedding-Worthy Pants

Comments

comments


Post navigation


Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com