MABOGA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Boga La Nazi 

Vipimo:

Boga – 1

Tui La Nazi – 2 Vikombe

Sukari – 1 kikombe

Hiliki – 1/2 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha na Kupika

  1. Unamenya maboga kiasi ukipendacho.
  2. Unayakata kata vipande vidogo vidogo.
  3. Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.
  4. Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.
  5. Kisha unamimina tui la nazi.
  6. Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa

JUISI YA EMBE NA KARAKARA/PASHENI

JUICE

Vipimo

Passion fruit – 8

Embe – 6 za kiasi

Maji – kiasi

Sukari – kiasi upendavyo

Namna Ya Kutayarisha

  1. Kata passion fruit toa nyama weka mashine ya kusagia (blender) . Tia maji kiasi kisha saga na uchuje .
  2. Saga embe na maji kidogo kisha changanya na juisi ya passion.
  3. Tia sukari korogo ikiwa tayari

Comments

comments