VILEJA VYA NAZI
Mahitaji:

Vikombe –  4 nazi aina ya Dessicated
Kijiko – 1 kidogo Vanilla
Kopo moja la Maziwa matamu ya Condensed
Kijiko – 1 kidogo baking powder
Kijiko – 1 kikubwa siagi iyayushe
Na Icing sugar kikombe 1 kwa kupambia.

NAMNA YA KUTAYARISHA:-

Changanya vyote hivyo isipokuwa Icing sugar kwenye bakuli la mashini na usage mchanganyiko huo hadi upate donge laini

11168577_701187273320756_4767611989722062225_n

Nyambua donge hilo kiasi ya kuuunda vitonge vidogo kasha weka kwenye kalai la kuoka , finyilia kidonge hicho uunde umbo la biskuti

Endelea kufanya hivyo kwa vitonge vyote na panga biskuti hizo kwa kuzipa nafasi kila baada ya nyengine kwenye ilo kalai

11059488_701187619987388_7700790192824562727_n

Washa jiko la kuoka (oven)   umoto wa degrees 175 C na zioke biskuti hizo kwa dakika 15 au 20 au mpaka zianze  kubadilika rangi na kua rangi ya kahawia na harufu ya kuvutia

Ziache zipoe kiasi ndipo sasa uzihifadhi kwenye sahani na kwa kutumia kichujio, nyunyizia icing sugar kwa juu kwa kupambia

11223648_701187139987436_5775681876079014962_n

Zihifadhi kwenye mkebe  kwa kuchelea kulainika kwa upepo na vile vile kudumu kwa wiki…

Nakutakia matayarisho mema ya  Eid

VILEJA VYA NAZI

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com