Kama una mpango wa kusuka hivi karibuni na hujui usuke nini au ungependa kujua ni mitindo gani ipo kwenye chat kwa sasa upande wa nywele hizi styles tatu zimeonekana ku trend sana kwa sasa wengi wametokea kuzipenda na kuzisuka
Beyonce’s formation tour cornrows hizi ni zile Beyonce alisukaga katika tour yake ya formation, yeye alisuka ndogo ndogo zika sukwa sana lakini kwa sasa zimeingia mtindo huu wa kubwa kubwa, rahisi kusuka na rahisi kuzimaintain
Elizabeth Michael Cornrows, hizi zilikuwa zina sukwa mbili wanasuka ndogo ndogo halafu wanaunganisha mikia na rasta lakini zinakuwa mbili tu, tangu Eliza azisuke mtaani kumeonekana kuvutiwa nazo kwa sasa zinasukwa kilimanjaro kama alivyosuka Eliza.
Hii ya kusuka hatujui tuiitaje lakini nayo imeonekana ku trend mitandaoni na mitaani
Kama una ratiba ya kusuka weekend hii basi aina hizi tatu za rasta zinakuhusu tuambie umeipenda ipi kati ya hizo?