Inawezekana ukawa unakula haya matunda lakini hujui faida zake nyingine, unakula tu kwa sababu unayapenda. Ukiachana na utamu  zambarau zina faida nyingi katika urembo lakini pia katika afya, leo tunakuletea namna ambavyo unaweza kutumia zambarau kutibu aina mbalimbali ya vitu katika ngozi.

  • Hutibu Chunusi

 

 

Mbegu za zambarau ni tiba nzuri ya chunusi, unachotakiwa kufanya ni kuchukua mbegu kavu (zilizo kaushwa) za zambarau ponda kisha changanya unga wa mbegu hizo na maziwa ya ngo’ombe, paka eneo lililo athirika na chunusi kaa nayo kwa dakika 15 kisha uoshe kwa maji ya uvugu vugu.

Kumbuka huwezi kutibu chunusi papo kwa papo kwahio tiba hii itachukua muda mpaka uanze kuona matokeo, lakini pia paka mara kwa mara kwa matokeo ya haraka.

  • Kungarisha Ngozi

Kama una dark spot zilizotokana na chunusi au maradhi mengine ya ngozi, basi mbegu za zabibu ni jibu lako. Unachotakiwa kufanya ni kupata unga wa mbegu za zambarau, almond oil na rose water. Changanya mahitaji yako kwa pamoja kisha pakaa usoni, kaa nao kwa muda mpaka ukauke kabisa katika uso wako kisha osha na maji ya baridi.

Unaweza kufanya hizi mara mbili kwa week ilikupata matokeo bora

 

Comments

comments