Wanawake wengi tunapenda kusuka rasta mitindo tofauti tofauti maana kila siku inakuja mipya lakini  huwa tunapitia hili tatizo, wengi huwa tunawashwa sana na hizi nywele ni kwa sababu ya joto na kwa sababu nywele ni fake zimetengenezwa na chemical ambazo huwa hazizuii joto, basi zile nywele zilivyo nyingi kichwani zikipigwa na joto unapata muwasho kichwani lakini je ni namna gani unaweza kuzuia hili?

Apple cider vinegar au plain vinegar vinaweza kukusaidia.

Namna ya kufanya  kabla ya kusuka rasta zako

  • Mimina kikombe kimoja cha Apple Cider Vinegar au Plain Vinegar katika Sink,beseni au bakuli.

 

  • Changanya na maji ya uvugu vugu
  • chukua rasta unazo taka kusukia weka kwenye bakuli au sink

  • ziache zikae kwa 30min au lisaa limoja
  • utaona vitu vyeupe vinaelea katika bakuli, beseni au sink lako hizo ndizo chemical

  • baada ya hapo osha rasta zako kwa maji masafi mara mbili na ukaushe zikauke tayari kwa kuzitumia
Hair Tips – How To Make Your Braids Stop Itching

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com