Katika kipindi cha Mwezi Tukufu wa Ramadhani, mazoea yetu ya kila siku, mpangilio na matumizi yetu ya chakula yana badilika. Lakini tunatakiwa kujua kwamba mabadiliko ya ghafla ya kubadilika kwa mfumo wa kula chakula katika kipindi kirefu cha kufunga inaweza kuumiza ngozi zetu.

Njia sahihi ni kuhudumia ngozi yako ili kuepuka mikunjo, kuchanika, ngozi kudhoofu na dalili zote za kukosa majini mwilini kutokana na kufunga kwa muda mrefu

VIPI UTAHIUDUMIA NGOZI YAKO

Tuna shauri unywe glasi nane za maji ukisha fungulia

Kula matunda mengi

Osha na paka mafuta mara kwa mara katika ngozi yako.

 

Ukweli: mwili wa binadamu una chukua 50/60 asilimia za viviminika asilia kama maji, juice ya matunda na 20/30 asilimia ya soda

Kula kwa afya kuna matunda na vyakula vingi ambavyo vitakusaidia  kukarabati ngozi ilio kauka kurudi karika hali yake ya kawaida mfano: korosho na lozi zina mafuta ya asili naprotini ambazo zitasaidia kung’arisha ngozi yako

Matunda kama zabibu na tende pia yana sifika kwa kupambana na vitu vikali (kemikali) pia yana vitamin chuma, vitamin A,potasiamu na kalsiamu yanasaidia kuongeza optimum katika afya ya ngozi,matunda yanasaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Fanya yaliyo bora kutoka katika kufunga kwa kuongeza madini yaliyo na afya katika ftari na suhoor (daku)

Comments

comments