Wengi wetu tume kua tukihifadhi vipodozi vyetu katika majokofu (friji) ili visiharibike bila kujua kuna faida na hasara za kufanya hivyo, si kila kipodozi kina faa kuwekwa katika jokofu vingine ukiviweka una haribu ubora wake.

Vipodozi ambavyo vimetengenezwa kwa mafuta na siagi vina nafasi kubwa ya kuhifadhiwa katika jokofu kwa sababu kwenye joto vinayeyuka na kupoteza ubora wake haraka.

Jambo la kwanza muhimu ni kusoma maelezo katika kipodozi chako. Na jambo la pili hata kama ime ruhusiwa kukihifadhi katika jokofu basi uwe una kiangalia mara kwa mara ili kuhakiki hamna bakteria walio ingia katika kipodozi chako.

MUHUIMU Kuwa muangalifu hata kama ni kipodozi ambacho kina uwezo wa kuhifadhiwa kwenye jokofu vinaweza kubadilika na kuleta matatizo unapo vipaka

Vipodozi vya macho ni vizuri kuweka katika jokofu, vipodozi hivi vikiwa vimepoa yaani vina ubaridi ina saidia kukupa muonekano mzuri, kusaidia mzunguko wa damu na kuondoa weusi chini ya macho. Kufanya hivi hakuna madhara ya muda mrefu bali kuna faida hasa katika kipindi cha joto.

fb-share-eye-creams-and-serums

Vipodozi kama make up, manukato,na rangi za kucha

NARS

havifai kuwekwa kwenye jokofu, vina haribika ubora wake kama manukato yataganda, na make up si nzuri kuweka katika friji labda kama ni mafuta ya mdomoni yame yeyuka uweke kuyangandisha tena au wanja ni vema kuuweka katika friji dakika chache kabla ya kuuchonga.

 

Comments

comments