Leilan ni Mtanzania ambaye alikuwa India kujifunza maswala mazima ya make up,Leilan ambaye kwasasa amerudi nchini Tanzania akiwa amefungua darasa la kufundisha maswala ya make up pamoja na urembo kwa ujumla.

Akiongea na Afroswagga ofisini kwake Tabata Segerea alisema “Nipo Tanzania natamani sana kufanya kazi na wasanii wa hapa lakini  changamoto niliyonayo ni kwamba hawanifahamu.Na kama akitokea msanii au wasanii basi mimi nipo tayari maana sichagui mtu wa kufanya nae kazi. Lakini India niliwahi kushiriki kufanya make up washiriki wa filamu ya Chamand Karoh na  Got talent hili ni tamasha kubwa pale india na make up nilifanya mimi. Pia kuna vitu vingi watu inapaswa watu  wajue hasa tofauti ya make za event na video music,ambapo tofauti ipo  katika event za kawaida inabidi utumie cream hasa, na video music utumie powder shauri ya camera zaidi lakini huwa naona watu wanajichanganya.

Naona hata mitaani wakina dada walio wengi wanapenda sana maswala ya kujua au kujifunza make up,lakini hawajui waende wapi.Mimi nipo wanaweza kuja muda wowote na kujifunza zaidi juu ya make up.”Alisema

Video chini  akiwa anamfanyia mmoja ya wadada make up.