Siku chache zilizo pita tuliuliza hili swali katika kurasa yetu ya Instagram ambapo watu wengi walijitokeza kujibu, kwanini tuliuliza? kwasababu sikuhizi tunawaona wadada/wamama wanabeba handbag kubwa na nzito mno hii ilitufnye tuwaze nini kipo katika handbags zao na amini usiamini huwa kuna vitu vingi mno vinabebwa kwa maana vilitajwa vitu vingi hadi tukawaza ni kweli mtu anatumia hivyo vitu vyote kila siku day in day out? au ndio ule uvivu wa kuvitoa na kuvirudishia kila mara? kwetu sisi tuna hisi inapaswa wanawake wakawa na ratiba ya kubeba vitu kwenye handbag zao, pale kitu kinapo hitajika kubeba basi ni vyema kikabebwa lakini kama si lazima kubebwa kwa siku hio basi kiachwe tu hadi pale kitakapo kuwa na uhitaji. Leo tunawaletea vile ambavyo ni muhimu kuwa navyo kila siku na vimetajwa kwa wingi katika post yetu.

  • Wallet – ni muhimu katika kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama pesa, vitambulisho, card za bank, picha nakadhalika hii inakufanya uwe na vitu muhimu katika sehemu moja na kujua kipi ukipate wapi na pia inapunguza mzigo katika hanbag yako

  • Khanga/mtandio – kama mwanamke/msichana nimuhimu kubeba khanga katika mkoba wako hujui nini kitatokea saa ngapi na wapi, nguo inaweza kuchanika ukajistiri kutumia khaga/mtandio wako.
  • makeup bag – makeup bag inasaidia kuweka makeup zakona vitu vyako vya urembo kama perfume, nail cutter, lip balms, lipstick, wipes,pads, makeups etc hii pia inakupa urahisi wa kubeba vitu vichache make up bags huwa ndogo fulani kuliko kutupia vitu tu kwenye handbag unaweza ukajikuta una hamishia dressing table nzima kwenye handbag lakini ukiwa na makeup bag unakuwa limited na unaanza kuchagua kipi muhimu kuwa nacho na kipi si cha muhimu.

  • note book ,pen,kitabu – hivi vitakusaidia katika kutengeneza to do list yako ya siku hio, kuwa na planned day saa ngapi ufanye nini nakadhalika.

kwetu hivyo ndivyo tulivyo viona ni muhimu kuwa navyo huitaji handbag kubwa au handbag iwe nzito kwa kubeba vitu ambavyo huna umuhimu navyo kila siku NOTE: ni vizuri kuwa unaangalia handbag yako mara kwa mara kubadilisha vitu vilivyopo ndani ya handbag yako kutokana na mahitaji yako.

Nini Kipo Katika Handbag Yako?

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com