Hakuna anayefurahia chunusi, na hakuna anayependeza akiwa na chunusi, Chunusi zimekuwa zikiwapata sana watu wenye ngozi za mafuta. Juhudi za kuteketeza mafuta yanayozidi kwenye ngozi zinahitajika kwani ndio chanzo kikuu cha chunusi.
Leo na waletea Apple cider vinegar (siki ya apple) kama kipodozi asilia cha kuzuia na kutibu chunusi.

Apple cider vinegar ina sifa ya kuua bakteria kwa haraka sana, pia ina sifa ya kukausha mafuta kwenye ngozi kwa haraka sana.Ila inashauriwa usitumie mara kwa mara maana kadri unavyokausha mafuta na apple cider vinegar ndivyo tezi za mafuta zinaongeza kasi ya kuzalisha mafuta yaliyokaushwa.
MAHITAJI
- Siki ya apple (apple cider vinegar)
- Maji safi
- Pamba
MATUMIZI
- Osha uso na maji safi,hakikisha uchafu wote umetoa.
- Changanya kifuniko kimoja cha siki kwa vifuniko vitatu vya maji.
- Chovya pamba kwenye mchanganyiko na upake maeneo yenye tatizo,kaa nayo kwa dakika 10 kisha osha.
- Fanya hivyo mara nyingi uwezavyo kwa siku.
- Pia unaweza kupaka na ukalala nayo usiku kucha.
- Hakikisha unapaka moisturiser baada ya kutumia.
Related posts
HOT TOPICS
Martin Kadinda Debuted She Gentle Collection At Swahili Fashion Week: Mbunifu Martin… https://t.co/BBAefWm0Al
FollowNjia Za Kujali Handbag Yako Idumu Muda Mrefu: Kama ambavyo unaweka cover na protector… https://t.co/rYXOb7PBbX
Follow#SwahiliFashionWeek2019 Lundi and Sons Collection #SwahiliFashionWeek2019 https://t.co/1sgnuYbDen
Follow
FOLLOW US!