Miguu ndio sehemu ambayo husahaulika sana, wengi wetu tukisha oga na kuipaka mafuta basi siku imeisha hatuijali kama sehemu nyingine za mwili lakini nani asiependa kuwa smooth mwili mzima? hamna si ndio? inawezekana tunaisahau kwa sababu product zake si nyingi kama viungo vingine lakini unaweza kutengeneza hii scrub nyumbani na ikakupa matokeo mazuri tu.

Mahitaji 

Limao – 1

Mafuta ya nazi – nusu kikombe

Sukari – kikombe kimoja kizima na robo kikombe

Kijiko na bakuli

 

Namna Ya Kufanya 

Kamua limao zima katika bakuli lako, kisha changanya sukari na mafuta ya nazi katika hilo hilo bakuli lenye juice ya limao baada ya hapo changanya mpaka mchangiko wako uchanganyike vizuri, kwa kutumia mikono paka mchanganyiko wako miguuni na usugue kwa muda kisha osha miguu kwa maji, jikaushe na upake lotion yako.

 

Sukari, Limao & Mafuta Ya Nazi Kwa Miguu Laini

Comments

comments


Post navigation


Leave a Reply

Social Media Auto Publish Powered By : XYZScripts.com