Kwa sasa kinacho trend katika ulimwengu wa urembo ni hat’s watu maarufu na mafashionista wameonekana kuvalia aina hii ya kofia kuweka statement katika mitoko yao, tuliziona katika run way mbalimbali za wabunifu na sasa zimeonekana kutrend sana kwenye swala zima la fashion.

Hizi sio tu zile kofia za kawaida unahitaji moja ambayo ipo unique na kukufanya u-make statement, the cartwheel hat zinavaliwa upande na hizi zilianza kuonekana kuwa popular miaka ya 1910 lakini zimekuwa most closely associated with 1940s-50s fashion. Well we all know fashion zinakuja na kupotea

Beyonce amekuwa akionekana anazivaa sana yeye anapendelea kuvaa kofia hizi na full outfit, kwenye tour yake ya otr2 ameonekana kuzitumia sana lakini tulishamuona miezi michache nyuma katika tuzo za grammy’s akiwa amevalia kofia ya aina hii pia.

Lakini we spotted rapper Cardi B katika Paris Fahion Week na yeye amevalia hii kofia kama ambavyo Beyonce anapenda kuvaa na yeye alimatch kofia na gauni lake & oh boy cardi slayed our souls.

Muigizaji kutoka Ghana, Nana Akua Addo na yeye hakuwa nyuma katika kufuata trend hii yeye alionekana akiwa katika location ya photoshoot ambapo kama Beyonce na Cardi B na yeye alivaa matching dress na hii kofia, its called taking notes.

Fashion bloggers nao hawapo nyuma ambapo tuliwakilishwa na huyu blogger kutoka Florida, Kerry Ann Scott-Spence yeye nae akiwa amevaa kofia hii nyeusi na outfit nyeusi.

Well we can’t wait to see our Tanzanian slayers on this trend.