Inawezekana wakati bado ana mwili mnene Wema alimiss kuvaa skinny jeans kwa maana kwa sasa ndiyo vazi lake kubwa, tunaweza kusema na flat tummy yake na suruali hizi zinamkaa vizuri lakini tatizo linakuja miguuni Wema ana skinny legs ( which is totally okay to have).

Ukiwa na skinny legs ukivaa skinny jeans hazikai vyema hasa kwa sababu zinachora miguu yako ilivyo na kukuonyesha juu mnene chini mwembamba. Hapa

Hii hai-apply tu kwa Wema lakini kama na wewe una miguu mwembamba na hujui uwekeze katika aina gani ya suruali ama suruali zipi zitakupa muonekano mzuri basi hii inakuhusu pia.

  • High Waist Wide Legs Trouser

Hizi zinafaa sana iwe una tumbo kubwa au dogo, iwe una tako au lah zinafaa ukizivaa zinakupa proportion tumboni huku ikificha miguu yako kwa kuwa chini ni pana.

  • Straight Legged Pants

Hizi ni zile suruali ambazo zipo straight mpaka chini, suruali hizi zinabana mapaja na kuachia chini lakini haziiachii sana kama bwanga hizi ni nzuri katika kuonyesha shape yako lakini pia kuficha wembamba wa miguu yako.

  • Mom Jeans

Mom jeans zinafaa sana kama unamiguu mwembamba hizi huwa ni high waist na pia ni straight miguuni kama ambavyo ilivyo kwa bwanga mom jeans zinakupa waist proportion na kuficha miguu yako vyema

Well Afromates ni matumaini yetu tumekusaidia kwa namna moja au nyingine tafadhali tuandikie ungependa tuandikie nini kingine katika segment hii ya AfroFix.