SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Aina Za Viatu Unavyopaswa Kuwa Navyo Kujifunzia Kuvaa Viatu Virefu
AfroTipAndTricks

Aina Za Viatu Unavyopaswa Kuwa Navyo Kujifunzia Kuvaa Viatu Virefu 

Tumekuwa tukipata malalamiko mengi kuhusu wengi wetu kupenda kuvaa viatu virefu lakini tunashindwa kutembelea (no lies sisi wenyewe hili ni tatizo kwetu pia). Viatu virefu kama bado huja vi-master ni tatizo unaweza kuanguka, kujikwaa mara kwa mara, miguu kuuma, kutokuwa comfortable wakati unatembea etc.

Wengi wetu huwa tunataka ku-skip kujifunza kidogokidogo na kutaka tuanzie kujifunza kutembelea viatu hivi kwa kununua viatu virefu lakini kumbe kuna viatu unaweza kununua na ukaanza navyo taratibu huku ukiongeza inch by inch pale ambapo unaona ume-master kutembelea inch fulani. mfano unaweza kuanzia kutembelea na block heels zilepana, ukaja kitten heels zile nyembamba lakini fupi, ukaja wedges ndefu, ukaja 3 inch’s na kuendelea.

Leo tunakuletea aina za viatu ambazo unaweza kuvaa wakati unaanza kujifunza kuvaa viatu virefu.

Block Heels Hizi ni aina zozote zinaweza kuwa pointy toe block heels, inaweza kuwa strap sandals block heels etc. Hivi ni vile viatu vyenye kisigino kirefu kidogo lakini kipana vipo comfortable sana

Kitten Heels hivi huwa na visigino vyembamba lakini vifupi, hivi huwa vina urefu wa  3.5 centimeters (1.5 inches) mpaka 4.75 centimeters (1.75 inches), na vyenyewe ni rahisi kutembelea na vipo comfortable. Itakuwa unajiuliza au unasema lakini huu ni mtindo wa zamani, yes ni mtindo wa zamani lakini kwa sasa upo kwenye chat tumeona fashionistas wengi wakiwa wanavaa viatu vya aina hii akiwepo stylist Joujou Nyaki kutoka tanzania

Mid Heels hizi ni nyembamba na urefu wake ni wa size ya kati yaani si ndefu wala si fupi, urefu wake huanzia 2 inches – 3 inches si nzuri kwa kuanzia lakini kama unaweza kutembelelea kitten heels hazihaziwezi kukupa usumbufu sana.

Wedges, Boots with block heels au strap block heels hizi nazo zinafaa kuanzia nazo kwa maana zina kisigino kinene na zina balance ya kutosha kabisa

Well kwa wale ambao mngependa kununua hivi viatu vinapatikana dukani kwetu unaweza kututembelea online @afroswagga_thrift au unaweza kutembelea duka letu lililopo tabata aroma. Karibuni

Related posts