SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna 3 Za Kuipa T-shirt Yako Muonekano Mpya
AfroTipAndTricks

Namna 3 Za Kuipa T-shirt Yako Muonekano Mpya 

Wewe ni mpenzi wa kuvaa t-shirt? Lakini huwa unavaa namna moja au mbili tu na inaanza kuwa boring? Tukisema namna moja au mbili tunamaanisha kuchomekea na kuchomolea t-shirt yako kwenye suruali au skirt uliyovaa? Leo tunakuletea namna 3 unazoweza ku-style tshirt yako ukapata muonekano mpya na kuonekana wa tofauti

  1. Kunja Mikono

Hii style iliingia na wengi walikuwa wanafanya hivi walikuwa wakionekana wahuni, lakini ni style nzuri ya ku-upgrade muonekano wako na watu wengi maarufu huitumia style hii akiwepo Rihanna

2) Funga Fundo

Yes kama unavaa t-shirt kwenda sehemu ambazo zinaruhusu kuonyesha mgongo au tumbo basi unaweza kukunja fundo t-shirt yako mbele au nyuma na ukapendeza sana kama ambavyo tunamuona Kim Kardashian alivyo-style ya kwake.

3) Chomekea Upande Mmoja

Hii style inafaa sana pale ambapo hujui uchomekee au uchomolee, side tuck ina serve both sides unakuwa umechomolea upande mmoja na kuchomolea mwingine, fashionista’s wengi hutumia style hii katika looks zao.

Tuambie ni style ipi umeipenda kati ya hizi tatu na je utajaribu kuitumia?

Related posts