SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Njia Za Kuondoa Harufu Ya Kabati Katika Nguo
AfroTipAndTricks

Njia Za Kuondoa Harufu Ya Kabati Katika Nguo 

Mara kwa mara wengi wetu tumekuwa tukikutana na hii hali, ukitoa nguo kwenye kabati kwa sababu mbalimbali utasikia inanuka kama uvundo wengi wanaita harufu ya kabati. Hii inatokana na

 • Nguo kukaa kwa muda mrefu kwenye kabati bila ya kutolewa kupigwa na hewa
 • Kama kabati liliingia maji au tunaweza kusema mvuke wa kabati
 • Kama ulichanganya nguo zilizokauka na zisizokauka vyema

Well haka kaharufu huwa kanakera sana hata upige pass, hata upake perfume bado utakasikia tu. Huwa haiondoki unless uifue au utoe ipigwe na upepo.

Leo tunakuletea njia mbalimbali ambazo unaweza kufanya ili harufu hii isiwepo katika nguo zako au kabati lako

 • Tumble Dryer Sheets

Hizi zipo kama wet wipes lakini hizi zinatumika katika kufulia nguo au kuweka chini ya mto, unaweza pia kuziweka katika kabati lako na ukapata harufu nzuri kwenye nguo na kabati lako

 • Tumia njia ya kuning’iniza nguo zaidi kuliko kuzikunja

hii inasaidia nguo kupata hewa lakini pia kutokugusana sana na mbao za kabati

 • Epuka kuziweka nguo kwenye mbao kabisa

Unaweza kutumia gazeti au kitambaa kwanza chini ya kabati kisha nguo zako zikaja juu ya hilo gazeti/kitambaa incase huo uvundo ukitokea basi utaingia kwanza kwenye kilichopo chini kabla ya kufikia nguo zako.

 • Kama kabati lako la milango liache wazi mara kwa mara

Yes kabati nalo linahitaji hewa, unapolifunga joto likazini linatoa mvuke ambao unakuja kusababisha majimaji na kulowanisha nguo ambapo inapelekea kupata uvundo. Liache wazi mara nyingi unavyoweza ili hewa iingie.

 • Udi Au Karafuu

Weka Udi au Karafuu kwenye kikopo kisha weka katika kabati lako nyuma au sehemu yoyote iliyojificha harufu zake zitaenea kwenye kabati na nguo.

 • Maua ya asumini

hii ilitumika sana zamani lakini kuna wengine mpaka leo wanatumia ni njia rahisi na haina ghrama, weka maua ya asumini machache katikati ya nguo zako zilizopo kwenye kabati, na sahau kuhusu uvundo.

Related posts

3 Comments

 1. internetinės parduotuvės produktų puslapius

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/afrotipandtricks/njia-za-kuondoa-harufu-ya-kabati-katika-nguo/ […]

 2. Visit This Link

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/afrotipandtricks/njia-za-kuondoa-harufu-ya-kabati-katika-nguo/ […]

 3. buy magic boom bars online store

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/afrotipandtricks/njia-za-kuondoa-harufu-ya-kabati-katika-nguo/ […]

Comments are closed.