SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

FUTARI YA CHAPATI KWA MCHUZI WA KUKU
Afya

FUTARI YA CHAPATI KWA MCHUZI WA KUKU 

Vipimo

Vikombe Vinne (4) Vya Unga Wa Ngano Mweupe

Vijiko vi tatu vya samli

~vijiko viwili vya chumvi

vikombe viwili vya maji ya uvugu vugu

samli (mafuta) ya kupikia chapati

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1.                Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
  2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
  3. Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano hivi.
  4.                Finika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa kuufunika ili hewa isiingie.
  5.                Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
  6.                Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
  7.                Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
  8.                Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
  9.                Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
  10.              Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
  11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
  12.              Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi

img_0198

  1. Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva  upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress  na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.
  1. Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa  kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya  kila chapatti.

 Kidokezo  

Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonyanye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida.

Unaweza ku freeze chapati katika Freezer bags.  Kunja chapati  moja moja ziwe nusu.  Zifunike na Wax paper, kisha zitie kwenye freezer bags na uzihifadhi katika freezer.  Unapotaka kula, toa kwenye freezer na upashe moto katika Microwave.

MCHUZI WA KUKU

Chicken Ghee Roast (6) - 1

mahitaji:
Chicken marination:-
Kuku mzima
Chumvi kjk 1 cha chai
Mtindi vjk 2 vya chakula
Binzari ya manjano 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Ndimu 1
Vitunguu saumu 1/2 kjk cha chai
Tangawizi 1/2 kjk cha chai

Filling
Biringanyi 2
Viazi 2
Kitunguu maji 1
Nyanya 2
Hoho 2
Binzari nyembamba ya unga 1/2 kjk cha chai
Giligilani ya unga 1/2 kjk cha chai
Chumvi
Garam masala 1/2 kjk cha chai

Maandalizi:
Chukua mahitaji yote ya marination changanya pamoja kisha pakaza kwenye kuku kwa juu na ndani pakaza vizuri mchanganyiko wote kisha weka pembeni kwa masaa 3.
Katakata vitunguu maji, viazi, biringanyi, hoho na nyanya vipande vidogo dogo.
Kaanga kitunguu maji kwenye sufuria vikiwa brown weka binzari zote na  viazi kaangia kwa dk 5, weka maji kama vinashika chini. Weka nyanya funika iive kidogo kisha weka biringanyi na hoho. Wacha mpaka mboga zote ziive.
Chota mchanganyiko huo kisha weka ndani ya kuku.mjaze kisha chukua vijiti vya meno mshone kisha chukua mafuta pakaza kwenye bati ya kuokea.juu muweke kuku kisha mwagia mafuta kidogo kwa juu na oka moto wa 175c kwa dakika 45.

 

Related posts

3 Comments

  1. buy ayahuasca tea online video,

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/afya/futari-ya-chapati-kwa-mchuzi-wa-kuku/ […]

  2. 다시보기

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/afya/futari-ya-chapati-kwa-mchuzi-wa-kuku/ […]

  3. liberty cap mushroom habitat

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/afya/futari-ya-chapati-kwa-mchuzi-wa-kuku/ […]

Leave a Reply