SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

IFTAR: CHAPATI ZA MAJI KWA CHOROKO ZA NAZI
Afya

IFTAR: CHAPATI ZA MAJI KWA CHOROKO ZA NAZI 

CHAPATI ZA MAJI

Vipimo:

Unga wa ngano  – 2 vikombe (mugs)

Mayai  –   2

Chumv-  Kiasi

Kitunguu maji cha kiasi  – 1

Kotmiri – 2 misongo (bunch)

Mafuta au samli ya kupkia    –   Nusu kibakuli

Maji   –  3 Vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

ep2HC

 1. Tia maji na mayai kwanza katika mashine ya kusagia (blender) kisha
 2. Tia unga, chumvi usage ili unga uchanganyike.
 3. Mimina katika bakuli, ikiwa unga mzito, ongeza maji kama uwe mwepesi kiasi.
 4. Katakata kitunguu maji na kotmiri uchangaye.
 5. Weka kikaango kisichoganda (non-stick frying pan) katika moto na uteke unga kwa upawa wa duara uutandaze vizuri katika kikaango.
 6. Subiri mkate ukauke, ugeuze upande wa pili huku unaungandamiza na kuuzungusha mkate katika kikaango ili uive.
 7. Uinue kidogo utie kijiko kimoja cha supu, mafuta au samli.
 8. Kakaanga hadi mkate uive uwe rangi ya hudhurungia kama katika picha.
 9. Geuza tena mkate na ugandamize gandamize tena kama dakika moja uive vizuri upande wa pili bila ya kutia tena mafuta kisha epua uweke katika sahani. Au unaweza kuukunja kama katika picha.
 10. Endelea kupika mingine hadi umalize.

CHOROKO ZA NAZI

Vipimo

Choroko za kupaaza – 1 kikombe kikubwa (mug)

Kitunguu maji –  1 kimoja

Binzari ya manjano ya unga   -1/2 kijiko cha chai

Kitungu saumu(thomu/galic)    – 1 kijiko cha chai

Nyanya  –  1 moja

Pilipili nzima  –  1-2

Chumvi  –    kiasi

Nazi – 1 kikopo (400-500 mls)

Namna Ya Kutayarisha

hqdefault

 1. Osha choroko zako vizuri na zichemshe kwa maji ya kiasi tu hadi ziwive na zisivurugike.
 2. Katakata kitunguu maji vipande vidogodogo.
 3. Imenye nyanya maganda halafu iponde.

Namna Ya Kupika 

 1. Weka sufuria jikoni na moto wa kiasi tia mafuta kidogo.(kijiko kikubwa cha kulia)
 2. Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi kidogo
 3. Tia binzari ya manjano kaangia kidogo
 4. Kisha tia vitunguu thaumu kaanga kidogo.
 5. Halafu mimina nyanya iliyosagwa na chumvi kiasi.
 6. Acha ikaangike huku ukikoroga.(kama dakika 5-10 hivi)
 7. Kisha mimina choroko zilizoshemshwa changanya acha maji yakauke kiasi
 8. Mimina nazi na onja chumvi kama imekolea punguza moto acha nazi ichemkie, kiasi cha kuacha urojo wa kutosha.
 9. Mwisho katia pilipili ziwivie kiasi.

Zikisha kuwa tayari mimina kwenye bakuli lako tayari kwa kuliwa na chapati , wali  hata pita bread (mkate)

Related posts

3 Comments

 1. Learn More Here

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/afya/iftar-chapati-za-maji-kwa-choroko-za-nazi/ […]

 2. mikestreeservicecompany.com

  … [Trackback]

  […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/afya/iftar-chapati-za-maji-kwa-choroko-za-nazi/ […]

 3. Buy fn guns

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/afya/iftar-chapati-za-maji-kwa-choroko-za-nazi/ […]

Leave a Reply