SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JIKONI LEO SHURBA KWA VITUMBUA
Afya

JIKONI LEO SHURBA KWA VITUMBUA 

Vipimo

Nyamna Ya mbuzi ya mifupA -1 Kilo

*Ngano nzima  – ¼ kikombe

Shayiri zilizopaazwa  (quacker oats) za tayari  – ¼ kikombe

Kitunguu saumua(thomu/galic) na tangawizi – 2 vijiko vya supu

Kitunguu – 1

Mdalasini vijiti -2

Bizari ya jiyra (cumin powder/bizair ya pilau)- 1 kijiko cha chai

Bizari ya majano (haldi/kurkum/tumeric powder)    -1 kijiko cha chai

Pilipili manga – 1 kijiko cha chai

Kidonge cha supu – 1

Chumvi  – kiasi

Siki au ndimu -2 vijiko vya supu

Mafuta -¼ kikombe

Maji  kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

lentil soup

  1. Chemsha nyama kwa maji kiasi mengi, tia  chumvi, mdalasini, thomu-tangawizi na pilipili manga. Funika nyama ichemke hadi iwive nyama.
  2. Toa nyama nusu kutoka katika supu au yote ukipenda, kisha itoe mafupa yake na utie nyama katika mashine ya kupaaza (chopper). Isage kidogo kiasi cha kuvurugika isisagike sana. Weka kando.
  1. Tia shayiri  katika supu iache iwivie kidogo pamoja na supu baada ya kutoa nyamaKatika kisufuria kidogo,
  2. tia mafuta katakata kitunguu ukaange hadi kianze kugeka rangi,
  3. tia bizari ya haldi na jiyra na endelea kukaanga kidogoIrudishe nyama katika supu, kisha tia kitunguu ulichokaanga, tia kidonge cha supu, tia siki au ndimu iache kidogo tu ichemke ikiwa tayari.

vitumbua

Vipimo

Mchele –  2 mugs

Tui la nazi  –   2 mugs

Yai  –  1 kubwa

Sukari  – ½ mug

Hiliki   –  ½ kijiko cha chai

Hamira –  ½ kijiko cha chai

Unga wa ngano  – 2 vijiko vya chakula

Samli ya kupikia  (au mafuta)     kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

IMG_21951

 

  1. Osha na roweka mchele kiasi masaa kuanzia mawili au zaidi.
  2. Saga mchele na tui kwenye mashine ya kusagia (blender) mpaka uwe laini usiwe na chenga.
  3. Tia hiliki, hamira na unga wa ngano saga tena mpaka uchanganyike.
  4. Mimina kwenye bakuli na uache uumuke kiasi.
  5. Ukisha kuumuka changanya sukari na yai
  6. Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia  kila kitumbua.
  7. Mimina mchanganyiko kiasi kwenye kikarai maalumu cha kuchomea vitumbua.
  8. Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
  9. Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.

 

Related posts

3 Comments

  1. เว็บพนัน

    … [Trackback]

    […] Read More Information here to that Topic: afroswagga.com/afya/jikoni-leo-shurba-kwa-vitumbua/ […]

  2. dried liberty cap mushrooms

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/afya/jikoni-leo-shurba-kwa-vitumbua/ […]

  3. this contact form

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/afya/jikoni-leo-shurba-kwa-vitumbua/ […]

Leave a Reply