Afya ni hali ya kuwa vizuri au kujisikia vizuri kimwili au kiakili bila kusumbuliwa na maradhi yoyote, basi ukiwa na hali hiyo wewe ni mtu mwenye afya nzuri. Afya ya binadamu itaimalika zaidi kama atakuwa anafuatilia kanuni na taratibu za kujenga afya
Kuna njia nyingi za kufanya au kutunza afya yako iwe njema na nzuri na kufanya uepukane na magonjwa ya mara kwa mara.
Kuwa muangalifu katika chakula/mlo, hili ni jambo la kwanza katika yale mengi yanayochagia kujenga katika kuimarika zingatia zaidi katika chakula.Maana haiwezekani kuwa na afya nzuri kama hautaweza kuzingatia vyakula vya kula/mlo. Matumizi ya chumvi, sukari,mafuta ya kula, kupita kiasi yatakufanya ukose afya nzuri.Ni vyema kula zaidi mboga mboga na matunda, kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vyenye sukari, pia ni vyema kuwa na taratibu za kubadilisha chakula mara nyingi uwezavyo ili kuweza kujenga afya nzuri.
Ufanyaji wa mazoezi, tendo la kufanya mazoezi ni tendo muhimu linalopaswa kufanywa na kila rika ili kuendelea kuimarisha afya. Kuna aina nyingi za mozoezi ambazo ni wazi kila rika linaweza kushiriki na kujenga afya kwa wakati. Mazoezi yana faida nyingi katika maisha ya mwanadamu, kutokunenepa au kupunguza unene, kupunguze hatari ya kupata ugonjwa wa presha, kuendelea kuwa mwepesi, kulala vizuri, na hata kuongeza uwezo wa kufikiri kwa haraka. Hivyo ni vyema kutenga muda wako walau kwa dakika 60 kwa siku ukafanya mazoezi ili ujenge afya nzuri.
Kutenga muda wa kupumzika, kitendo cha kuwa na muda mzuri wa mapumziko hujenga afya njema, mara nyingi watu wamekuwa wakifanya kazi kupita kiasi hivyo kitendo cha kukosa muda wa mapumziko basi hupelekea kukosa afya njema.
Usafi, hakika afya njema na nzuri inaambatana na swala zima la usafi. Katika usafi ni vyema kuwa mwanagilifu zaidi katika matumizi ya vitu mbalimbali ni vyema kuhakikisha kama vina usafi wa wewe kuweza kutumia. Kama ukizingatia usafi wa mambo yote hakika utakuwa na afya inayoimarika kila iitwapo leo.
Story Credit @batro15
Related posts
2 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/afya/jinsi-ya-kutunza-afya-yako/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on to that Topic: afroswagga.com/afya/jinsi-ya-kutunza-afya-yako/ […]