SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MAANDAZI KWA NDIZI TAMU ZA NAZI
Afya

MAANDAZI KWA NDIZI TAMU ZA NAZI 

MAANDAZI

Vipimo

Unga  -5 Vikombe

Tui la Nazi zito vugu vugu –   1 ¼ kikombe

Sukari  –3/4 kikombe cha chai

Samli iliyoyayushwa au mafuta  – 3 vijiko vya Supu

Hamirah –  2 Vijiko vya Supu

Hiliki – 1/2 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

IMG_8830

  1.  Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya   kulia vya tui. Weka kando  mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
  2. Pasha samli moto
  3.  Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki  na   samli ikiwa bado moto moto.
  4. Mimina hamira  ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.
  5. Kata madonge *12 au 15  uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.

*Ukipenda  maandazi  manene fanya madonge 12.  Ukipenda mepesi fanya madonge 15

  1. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.
  2.   Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari

Vidokezo: Kuhifadhi Maandazi

  1. Unaweza kuweka unga wa maandazi uliyokwisha kuyakata ndani ya freezer yakisha umukua  ikiwa unataka kutumia siku nyengine. Tumia waxed paper na unga wa kutosha kuweka katikati ya maandazi ili yasishikane unapoya freeze kwanza katika freezer.  Yakishika barafu, toa na yafunike kwa wax paper kiasi kama matano pamoja na uyatie katika freezer bags.    Ukitaka kukaanga maandazi siku nyengine, toa maandazi mapema kidogo  yatoke barafu kidogo tu.  Pasha mafuta moto kwenye karai na kanga maandazi.
  2. Vile vile unaweza kuyapika kabisa na kuweka katika freezer bags, ukitaka kutumia ni kuyatoa tu na kupasha moto katika Microwave
  3. Madonge yakifura, sukuma kama chapati kisha ukate mara nne kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo na madonge yote. Yawache maandazi yafure tena baada ya kukata kama dakika 15 hivi.

 

Mahitaji

  • Ndizi tamu (plantain) 3-4
  • Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
  • Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
  • Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
  • Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho
IMG_4729

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futar

 

Related posts

1 Comment

  1. БИНАНС РЕГИСТРАЦИЯ

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/afya/maandazi-kwa-ndizi-tamu-za-nazi/ […]

Leave a Reply