-
Pakiti la macaroni 1
-
Pilipili manga (utaisaga)
-
Chumvi
-
Blue band / Tanbond
-
Nyama ya kusaga
-
Kitunguu maji kikubwa 1 (kikate vipande vidogo vidogo)
-
Vitunguu swaumu (utaviponda)
-
Tangawizi (utaiponda)
-
Viazi ulaya (vikate vipande vidogo vidogo)
-
Biringanya (ikate vipande vidogo vidogo)
-
Pilipili hoho (ikate vipande vidogo vidogo)
-
Pilipili kali (iache nzima)
-
Karoti (ikate vipande vidogo vidogo)
-
Nyanya 2 (zikate vipande vidogo vidogo)
-
Tui la nazi (binafsi napenda lile la kukuna na kukamua mwenyewe)
-
Tayarisha sufuria safi, weka maji ya kutosha
-
Ongeza chumvi kiasi na pilipili manga iliyosagwa
-
Weka jikoni na yaache mpaka yachemke
-
Ingiza macaroni kwenye maji yaliyochemka.
-
Japokua pakiti nyingi zinaandika kuwa muda wa kupika ni dakika 9 – 10, mi nashauri uhakikishe uivaji kwa kuzionja (unaweza kulisha watu kibichi)
-
Baada ya kuiva epua sufuria
-
Tayarisha chujio na mimina macaroni ndani ya chujio ili kuchuja maji uliyochemshia macaroni
-
Chukua maji yasiyo moto wala baridi miminia juu ya macaroni yakiwa bado ndani ya chujio
-
Rejesha sufuria uliyochemshia macaroni kwenye jiko huku ukiwa umepunguza sana moto
-
Weka Blueband/ Tanbond ndani ya sufuria yako na iacha iyeyuke vyema
-
Rejesha macaroni ndani ya sufuria yenye Blueband/ Tanbond
-
Waweza ongeza pilipili manga iliyosagwa kama ukipenda
-
Koroga vyema kwa dakika 2 ili mchanganyiko wa macaroni, pilipili manga na Blueband/ Tanbond ukolee vyema
-
Macaroni yako yapo tayari kwa kuchanganywa na mboga.
-
Epua sufuria weka pembeni na zima jiko
Tumalizie na Nyama ya kusaga:
- Tayarisha sufuria safi, weka nyama ya kusaga peke yake bila ya kuweka maji
- Ongeza chumvi kiasi, tangawizi na kitunguu swaumu
- Weka sufuria lenye huo mchanganyiko kwenye jiko na washa jiko
- Ongeza maji moto safi kila mara pale nyama inapokaukia
- Funikia sufuria ili nyama ipate kuiva taratibu, hakikisha nyama imeiva vyema (ionje kama imeiva)
- Baada ya kuiva epua nyama iweke kwenye chombo kingine pembeni.
-
Rudisha sufuria jikoni na weka mafuta ya kupikia kama vijiko vitatu
-
Ongeza chumvi kidogo, kisha weka vitunguu maji. koroga mchanganyiko huo (lazma utasikia harufu nzuri ya vitunguu vinaiva)
-
Vitunguu vikishaiva na kubadilika rangi ongeza pilipili kali moja bila kuikata
-
Ongeza vipande vya viazi na karoti na koroga
-
Ongeza biringanya, pilipili hoho na mchuzi ambao utakua upo katika ile nyama tuliyochemsha
-
Ongeza viungo kama vile vya pilau n.k (hapa inategemea unapenda viungo vipi, maana vipo vingi)
-
Vikishaiva ongeza nyanya, na ukorege kiasi kisha acha vichemke kidogo ili kutengeneza rojo
-
Weka nyama ya kusaga koroga vizuri huo mchanganyiko kisha acha kidogo vikolee
-
Waweza weka Royco mchuzi mix kama utapenda (mimi niliweka) kisha korogo rosti hilo
-
Malizia na tui na hakikisha unakoroga tui lisije kata
-
Baada ya tui kuiva vyema epua mboga yako tayari kwa kuchanganya na macaroni na kuliwa
-
Chukua chombo kingine tofauti, kikavu na kisafi (hotpot inafaa sana)
-
Weka macaroni yako kidogo, kisha unaweka mboga ya nyama ya kusaga kidogo kidogo huku unakoroga
-
Hakikisha macaroni na nyama vinachanganyika vyema.
-
Pakua chakula chako tayari kwa kuliwa.
- Tayarisha sufuria safi, weka nyama ya kusaga peke yake bila ya kuweka maji
- Ongeza chumvi kiasi, tangawizi na kitunguu swaumu
- Weka sufuria lenye huo mchanganyiko kwenye jiko na washa jiko
- Ongeza maji moto safi kila mara pale nyama inapokaukia
- Funikia sufuria ili nyama ipate kuiva taratibu, hakikisha nyama imeiva vyema (ionje kama imeiva)
- Baada ya kuiva epua nyama iweke kwenye chombo kingine pembeni.
- Rudisha sufuria jikoni na weka mafuta ya kupikia kama vijiko vitatu
Ongeza chumvi kidogo, kisha weka vitunguu maji. koroga mchanganyiko huo (lazma utasikia harufu nzuri ya vitunguu vinaiva)Vitunguu vikishaiva na kubadilika rangi ongeza pilipili kali moja bila kuikataOngeza vipande vya viazi na karoti na korogaOngeza biringanya, pilipili hoho na mchuzi ambao utakua upo katika ile nyama tuliyochemshaOngeza viungo kama vile vya pilau n.k (hapa inategemea unapenda viungo vipi, maana vipo vingi)Vikishaiva ongeza nyanya, na ukorege kiasi kisha acha vichemke kidogo ili kutengeneza rojoWeka nyama ya kusaga koroga vizuri huo mchanganyiko kisha acha kidogo vikoleeWaweza weka Royco mchuzi mix kama utapenda (mimi niliweka) kisha korogo rosti hiloBaada ya tui kuiva vyema epua mboga yako tayari kwa kuchanganya na macaroni na kuliwa
-
Chukua chombo kingine tofauti, kikavu na kisafi (hotpot inafaa sana)Weka macaroni yako kidogo, kisha unaweka mboga ya nyama ya kusaga kidogo kidogo huku unakorogaHakikisha macaroni na nyama vinachanganyika vyema.
-
pakua tayari kwa kuliwa
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] There you can find 62420 more Info on that Topic: afroswagga.com/afya/makaroni-na-nyama-ya-kusaga/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/afya/makaroni-na-nyama-ya-kusaga/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/afya/makaroni-na-nyama-ya-kusaga/ […]