SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MKATE WA UFUTA KWA SAMAKI WA KUPAKA
Afya

MKATE WA UFUTA KWA SAMAKI WA KUPAKA 

MKATE WA UFUTA

Vipimo:   (vya kutokea mikate  6)

Unga – 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Tui la nazi au maziwa     – 2 ½

Hamira  –  1 Kijiko cha supu

Chumvi    -Kiasi

Sukari    -1 kijiko cha chai

Yai  –  1

Ufuta  –     Kiasi

Mafuta au samli Ya kupakia mkate  –    Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1)   Changanya pamoja unga, nazi, chumvi, hamira, sukari na yai.  Hakikisha unga wote umetoka madonge na umevurugika vizuri uwe laini. (uwe maji maji kama wa kaimati lakini unakuwa mzito kidogo kuliko wa kaimati).

2)   Usubiri uumuke (Ufure)

Jinsi Ya Kuchoma Mikate:

RECIPE-0216-Naan

1)   Hakikisha chuma cha kuchomea kiwe kinagandisha vizuri (Kisiwe non- stick) na pia kisiwe kilichopikiwa mafuta.

2)   Weka chuma  kwenye moto, kikipata moto rushia maji ya chumvi kidogo halafu tia unga  kiasi kama kiganja kimoja cha mkono, utawanye vizuri kwa vidole halafu nyunyizia  ufuta juu yake.

3)   Ukianza kuwa mkavu nyanyua chuma   kifudikize  kwenye moto mpaka mkate wako uwe rangi ya dhahabu.

4)   Toa kwenye chuma kwa kutumia kisu.

5)   Paka samli au mafuta juu ya mkate  kwa tumia brush.

6)   Endelea hivyo hivyo mpaka umalizie unga wote.

 

SAMAKI WA KUPAKA

Vipimo

Vitu Vya Samaki

Samaki mkubwa wa chango –   1

Thomu na Tangawizi iliyosagwa  – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagawa  –  1 kijiko cha supu

Bizari ya pilau ya unga –   ½  kijiko

Ndimu –     1 kamua maji

Chumvi

Vitu Vya Rojo 

Vitunguu maji – 2

Nyanya –   2

Tuwi la nazi zito   –  1 ½  kikombe

Nyanya ya kopo  –  1 kijiko cha chai

Bizari ya manjano – ½ kijiko cha chai

Pilipili mbuzi  –    1 au mbili

Ndimu-  1 kamu maji

Chumvi –    kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

12a11d1bdd1da484284dd08a99b73bbdefc8202d

 1. Mroweke samaki kwa viungo hivyo kisha muweke katika tray na mchome (grill) katika jiko (oven), akiwiva upande  mmoja mgeuze upande wa pili.
 2. Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika  mashine  (blender). Na ukipenda iwe kali zaidi  tia pia  pilipili mbuzi moja, kisha mimina katika sufuria utakayopikia.
 3. Tia tui na bizari zote pamoja na nyanya ya kopo, chumvi, pilipili mbuzi nzima na pika moto mdogo mdogo.
 4. Rojo likianza kuwa zito tia ndimu.
 5. Epua na mwagia juu ya samaki.  Tayari kuliwa.

Related posts

6 Comments

 1. you can try these out

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

 2. เว็บตรง betclic88

  … [Trackback]

  […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

 3. buy pills online

  … [Trackback]

  […] There you will find 11860 more Information on that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

 4. weed delivery richmond hill

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

 5. where can you buy mushrooms in denver

  … [Trackback]

  […] Read More Info here on that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

 6. join illuminati

  … [Trackback]

  […] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/afya/mkate-wa-ufuta-kwa-samaki-wa-kupaka/ […]

Leave a Reply