SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Selfcare Ideas To Try This Weekend
Afya

Selfcare Ideas To Try This Weekend 

Inawezekana umeshakutana na hili neno huko mitandaoni lakini hujajua maana yake ni nini “Selfcare”, Selfcare ni hatua za kuchukua muda kujiangalia/kujihudumia wewe mwenyewe, mara nyingi huwa tunajisahau tunaangalia afya za wengine kuliko sisi wenyewe au tunaweka muda wetu mwingi kwenye kazi/biashara/kutafuta pesa na mahitaji mengine na kujisahau kujitunza wenyewe.

Kuna aina nyingi za selfcare mfano ni:

  • Social Self-Care.
  • Mental Self-Care.
  • Spiritual Self-Care.
  • Emotional Self-Care
  • Physical Selfcare

Sisi leo tunaangalia sana kwenye physical ambayo hii inahusiana zaidi na muonekano pamoja na mwili, unapoutunza mwili wako basi utafikiri na kujisikia vizuri pia. Kujitunza kimwili ni pamoja na jinsi unavyoupa mwili nishati, muda unaopata wa kulala, ni kiasi gani cha shughuli za kimwili unazofanya, na jinsi unavyoshughulikia mahitaji yako ya kimwili. Hapa kuna baadhi ya maswali unaweza kujiuliza ili kutathmini afya yako ya kimwili

  • Je, ninapata usingizi wa kutosha?
  • Je, mlo wangu unachochea mwili wangu vizuri?
  • Je, ninasimamia afya yangu?
  • Je, ninafanya mazoezi ya kutosha

Baada ya kujua hayo yote na kama unayafanya vyema basi vizuri na kama huyafanyi vyema basi jaribu kubadilika, mambo mengine ambayo unaweza kufanya ni pamoja na

Kula Chakula Chenye Afya (Healthy Food)

  • Siku za kawaida inawezekana unakula chochote tu ili mradi upate kula lakini hii weekend ukiwa umepumzika jaribu kuangalia nini unakula na ikiwezekana plan chakula chako cha week nzima ili usije ukala chochote tu kisichokuwa healthy.

Jali Ngozi Yako

  • Kama ilivyo kwenye kula ngozi pia huwa tunaziburuza tu tukiwa na haraka zetu za kwenda shughulini, weekend hii chukua muda wako kujali ngozi yako, fanya skincare, kama unaweza nenda spa.

Fanya Mazoezi

  • Ni muhimu hasa kwenye kutengeneza mwili na ngozi lakini pia inasaidia kukufanya uondoe uchovu wa week nzima na kuondoa mafuta ambayo ulikula week nzima, pia inasaidia kuchangamsha akili na ukaanza week yako vyema kabisa.

Safisha Kabati Lako

  • Safisha kabati lako inawezakana week nzima ulikua unatupa tupa tu nguo, hakikisha unalisafisha na kutoa vyote visivyo vaa, panga unavaa nini week ijayo, itakupunguzia stress za asubuhi lakini pia kuvaa vyema kunakufanya ujisikie vizuri.

Mkawe na week njema na tuambie je wewe huwa unatumia weekend yako kufanya nini katika selfcare?

Related posts