SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

TIBA YA MAJI KWA AFYA YAKO
Afya

TIBA YA MAJI KWA AFYA YAKO 

Leo tushirikiane hii water therapy, sote tunakunywa maji lakini tunatofautiana namna tunavyotumia kinywaji hiki. Mara nyingine unaweza kuwa na tatizo aidha kusumbuliwa na kichwa, uchovu, kupoteza mng’ao wa ngozi au hata tumbo kutokaa vizuri kutokana na gesi n.k na mtu akakuambia tu kunywa maji mengi bwana au haunywi maji ya kutosha lkn kumbe sio tu kunywa maji mengi: ni unakunywa maji mengi kwa mpangilio upi?!

Jaribu kufuata mpangilio huu ;

Asubuhi
Kabla hujaweka mdomoni chochote kunywa maji si chini ya lita moja ndani ya dakika chache, ideal na Maximum ni lita moja na nusu tumbo lijae ‘ndi’ achana na kichefuchefu utajisikia vizuri si muda mrefu. Ukishakunywa ukamaliza tu haya maji utajisikia utumbo umeamka utapata haja kubwa. Baada ya hapo endelea na ratiba zako zingine kama ni kuoga,mazoezi n.k kunywa kifungua kinywa chako baada ya dakika 45 au saa 1.

Masaa kadhaa baada ya kifungua kinywa na kabla ya mlo wa mchana
Muda huu utakunywa maji nusu lita (500mls) hadi  robo tatu lita(750mls).
Iwapo yale maji ya asubuhi ulikunywa saa 12 had saa1 hivi basi mpaka saa 5 utakuwa umekojoa hata mara tano mkojo usio na rangi yaani kama maji, baada ya hapo utaanza kuwa na rangi. ukiona unaanza kuwa na rangi basi ni wakati wa kunywa maji mengine.

Alasiri
Muda huu utakunywa maji nusu lita (500mls) hadi  robo tatu lita(750mls).
Baada ya mlo wako wa mchana usinywe maji. Baada ya saa moja au mawili ukiendelea na zoezi la kukojoa maji uliyokunywa kabla ya mlo unaweza kunywa maji mengine. hii inaweza kuwa saa 9 hadi saa 11 jioni.

Usiku
Unaweza kunywa maji kiasi tu mradi usinywe wakati unakula.

Unafaidikaje kwa kupangilia hivi unywaji wa maji mengi wakati huo huo?

  • Unaamsha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula asubuhi hivyo chakula kilichosimama katika mfumo kinatolewa nje ili kisiendelee kuchacha na kuzalisha bacteria wabaya.
  • Unapunguza tindikali (asidi) zinazoweza kuwa zimechochewa baada ya chakula kukaa muda mrefu tumboni.
  • Unapunguza uzalishaji wa gesi tumboni, tumbo kujaa gesi au kujisikia umeshiba sana.
  • Unachangamsha mwili wako.

Baada ya muda mrefu wa kutumia maji namna hii unafaidikaje?

  • Kuwa na ngozi inayong’aa kwa kuwa na afya, pia kupungua/ kumaliza chunusi maana viwango vya maji na mafuta kwenye ngozi vinakuwa katika uwiano. Hydration is the key.
  • Unajisikia u mwepesi maana mwili unakuwa haushikilii maji maana maji yanakuwa mengi katika mifumo yako.
  • Kuweza kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
  • Kuweza kupungua uzito au kudhibiti uzito.
  • kupunguza sumu mwilini hasa zinazotokana na madawa na vyakula
  • Kupunguza uwezekano wa maambukizi ya mara kwa mara katika mfumo wa mkojo.

Kutokana na majukumu ya kila siku saa zingine inakuwa ngumu kunywa maji mengi hasa kutokana na usumbufu wa kwenda msalani mara kwa mara na foleni za barabarani n.k, unaweza kuamka ukajiandaa kwenda kwenye shughuli zako ukiwa na maji yako umebeba ukifika unakoenda kunywa maji yako kwanza ndo uendelee na kazi hii utaepuka usumbufu wa kukojoa wakati upo njiani kwenye foleni.

Pia unaweza kuchagua siku chache katika wiki ambazo utakuwa unakunywa maji kwa mtindo huu, mfano unaweza kufanya Jumatatu,Jumatano na Ijumaa au ukafanya jumanne na alhamisi au ukafanya weekend.
Ukiwa katika water therapy ili kupata faida epuka kabisa matumizi ya vinywaji vyenye sukari.
Kunywa maji ya joto la kawaida, usinywe ya baridi sana (yaliyotoka kwenye fridge).

Tufollow Instagram @afroswagga

Twitter @afroswaggatz

na facebook AfroSwagga

Related posts

4 Comments

  1. molly drug song lyrics,

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/afya/tiba-ya-maji-kwa-afya-yako/ […]

  2. Golden Teacher Mushrooms for sale New South Wales

    … [Trackback]

    […] Find More to that Topic: afroswagga.com/afya/tiba-ya-maji-kwa-afya-yako/ […]

  3. Darknet market links list 2023

    … [Trackback]

    […] Here you will find 76242 more Info to that Topic: afroswagga.com/afya/tiba-ya-maji-kwa-afya-yako/ […]

  4. 티비위키

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/afya/tiba-ya-maji-kwa-afya-yako/ […]

Leave a Reply