SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Vitu Vya Kubeba Ukiwa Kwenye Hedhi
Afya

Vitu Vya Kubeba Ukiwa Kwenye Hedhi 

Kukabiliana na kipindi hiki cha mwezi huwa ngumu w kwa mwanamke yeyote k, lakini mambo machache yanaweza kuleta tofauti kubwa linapokuja suala la kufanya hedhi yako iwe rahisi kukabiliana nayo.

Mfano ukiwa unajua siku zako na kuanza kujiandaa mapema itakuletea urahisi lakini pia namna nyingine ya kukabiliana na hali hii ni kubeba vitu sahihi, tunajua kila hedhi huja kitofauti hii inakuwa na hasira hii na furahi, hii inaweza kuwa chache na nyingine nyingi basi hivi vitu vichache vitakavyo kusaidia kufanya hedhi yako iende kwa urahisi:

Pad Ya Ziada

Hakikisha kwenye handbag yako una pad ya ziada maana inaweza kuanza muda wowote au kuchafuka ikakubidi ubadilishe pad yako, ukiachana na sababu hii ya kuchafuka pia ina shauriwa ki-afya ubadilishe pad kila baada ya masaa 3-4.

Extra Panties / Clothes

Kwa wale ambao tunaenda maofisini au mizungukoni ni vyema ukabeba nguo ya ndani ya ziada na vazi la nje la ziada incase ukichafuka uweze kubadilisha.

Disposable Bag / Tissue

Unapokuwa hedhi na unataka kubadilisha pad yako unaweza kwenda sehemu hawana vyoo vya kuchuchumaa na dustibin ni vyema ukabeba kijimfuko kidogo ambacho utawekea pad yako chafu lakini pia unaweza kuweka humo ndio utupe, hii itakufanya uwasaidie na wengine hasa wale wasafisha vyoo kutokuona damu zako.

Dawa

Hedhi huwa hazina utaratibu maalum unaweza kuumwa mwanzo, katikati au hata mwisho wa hedhi inakuja tu yenyewe inavyojisikia ni vyema ukawa na dawa mfukoni pale inapotokea unaumwa unaweza kijitibu.

Perfume

Hedhi zinaweza kuwa smelly at times na wengine kipindi hiki wanakuwa na kiarufu kisicho ridhisha basi beba manukato yako pale unapojihisi una sikia harufu sio nenda uwani jisuuze kisha ujipulizie perfume. Kama harufu yako inatoka kwenye makwapa na hauna namna ya kuoga basi beba wet wipes jifute na ujipulizie manukato.

Related posts