Tuzo za Mtandaoni za Afroswagga (Afroswagga Online Fashion Awards- AsOFA) zilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 zikiwa na lengo la kuongeza chachu katika tasnia ya mitindo na ubunifu nchini Tanzania. Mtandao umekuwa na nguvu kubwa katika kuchochea ukuaji wa sekta hii ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ikisuasua, kupitia mitandao ya kijamii tumepata kuona namna inavyoshika kasi siku hadi siku. Hivyo basi Afroswagga imeamua kutumia jukwaa la mtandao kufikia watu wengi zaidi katika kutoa tuzo.


Vipengele vya tuzo


Mwaka 2019 kulikuwa na jumla ya vipengele 16 katika tuzo zetu. Pamoja na ongezeko la kipengele 1, tunafahamu vipo vipengele vingine vingi ambavyo vinastahili kuwepo. Lakini tutaendelea kuviongeza taratibu kwa kuzingatia maoni na mapendekezo yako ukiwa kama wadau wa sekta hii.WASHIRIKA

Mwisho wa safari moja, ndio mwanzo wa nyingine. Katika mwaka huu wa 2020 tunakaribisha mtu nafsi/chapa (brand) watakao/zitakazo penda kuwa sehemu ya tuzo kama washirika/wadhanimi. Wasiliana nasi kupitia +255 785 554 518 au tuandikia barua pepe Afroswagga Awards kufahamu zaidi.