Katika hiki kipengele cha fanya mwenyewe tuna waletea vitu ambavyo unaweza kufanya mwenyewe kirahisi na nafuu, ni vitu ambavyo unaweza kufanya ukavaa au kugeuza biashara.
kwa sasa vitu ambavyo vinapendwa zaidi ni vitu ambavyo vya kipekee, watu wengi hawapendi kuvaa vitu ambavyo mwingine nae anacho, unaweza kutumia mfano huu au kuongeza vyovyote ambavyo unahisi utapendezewa
MAHITAJI
Chupio – 10
Rangi za kucha upendazo kulingana na mahiyaji yako
Mkasi
Waya
Vitu hivi una weza kuvipata popote kwenye maduka ya urembo na havigharimu zaidi ya shilingi 5000 (elfu tano) ya kitanzania.
JINSI YA KUTENGENEZA
1) Weka chupio zako zote kumi katika kipande cha boksi au sahani kwa mtindo wa kusimamisha
2) zikiwa katika mtindo huohuo wa kusimamisha zitenganishe kwa mafungu mawili yaani tano tano
3) anza kupaka rangi kwa mtindo utakao kama ni bendera, pundamiria au vyovyote vile upendavyo
4) rudia kupaka rangi mara nyingi uwezavyo pande zote mbili za chupio mpaka utakapo ridhishwa na muonekano wa chupio zako
5) ziache zikauke kwa usiku mzima
6) Zikisha kauka anza kutengeneza kishikio cha chupio zako ili kuweza kuzivaa
6) ingiza chupio zako katika hiko kiwaya na ukifunge
7) na kisha weka kivalio cha hereni
Hereni zako zipo tayari kuvaliwa
Mifano Mingine
Related posts
HOT TOPICS
Happiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/VZ1jH2zJUg
FollowHappiness Magese Akionyesha Wanawake Warefu Namna Ya Kuwa Stylish: Kwa wanawake warefu huwa… https://t.co/689j7Yjcn0
FollowSubscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
Feza Kessy Atuelezea Kuhusu Fashion & Style Zake
Feza Tadei Kessy ni Muimbaji, Muigizaji lakini pia ni mtunzi wa nyimbo lakini pia Fezza ni former beauty queen ambapo mwaka 2005 alikuwa Miss Dar City Centre, Miss Ilala & Miss Tanzania Runner up. Lakini pia alishawahi kuwepo katika Reality Tv Show – Big Brother Africa. Kwa…