SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

3 Bad Posture To Fix For Confident Body Language
Dondoo

3 Bad Posture To Fix For Confident Body Language 

Kama kuna vitu ambavyo hatufundishwi hasa sisi wa-Africa ni kuhusu kujiamini na body language, kwetu tembea utakavyo, kaa upendavyo ni wewe na maisha yako lakini kumbe kuna namna ambavyo tunatakiwa kufanya vitu hivi tunapoenda mbele ya watu wanaojua hivi vitu wana tutafsiri vibaya kama hatuna heshima au hatujiamini kumbe ni vile tu hatujui kwamba hiki kitu kinamaanisha nini kwa wengine.

Je posture gani ambazo unatakiwa ku fix ili uonekane una jiamini?

  • Kukaa Huku Umepinda Mgongo

Nna uhakika asilimia 90 ya tunaosoma hapa tumekaa huku tumepinda mgongo, hivi ndivyo mazoea yetu lakini kumbe unatakiwa ukae ukiwa umenyooka na kurelax kama umeshawahi kusikia watu wakisema huyu anakaa kama miss, basi ule mkao si wa mamiss tu bali mtu yoyote ana paswa kukaa vile.

  • Kuinama mbele unapotembea

Hii pia ni moja ya tabia ambayo wengi tunayo unatembea huku umeinama mbele au umeinamisha uso chini, badala yake tembea ukiwa umenyooka, mabega yarudi nyuma kidogo na usiinamishe sura chini, umeshawahi kusikia watu wakisema anatembea kwa kujiamini? anatembea kama ana imiliki Dunia? basi huu ndio muondoko unaotakiwa na mara nyingi tunaona zaidi kwa mamiss au watu maarufu.

  • Kusimama Ukiwa Umepinda Mgongo

Jifunze kusimama straight bila kupinda huku mabega yako yakiwa nyuma namna hii utapata muonekano wa kujiamini zaidi, angalia picha kujua tunaongelea nini.

Related posts