Japo kuwa na kuwa hizo dondoo 7 lakini bado muda mwingine unaweza kupata shida kuwa stylish, saa nyingine una hitaji msaada kutoka kwa watu tofauti tofauti. Watu kama Wema, Jokate au Lulu wanwavutia wasichana wengi kwa jinsi ambavyo wako stylish lakini hao wasichana hawajui ni nini wafanye na wengine hudhani wana hitaji hela nyingi kuwa Stylish fuatisha haya machache,
7) JUA RANGI ZIPI ZINAKUPENDEZA ZAIDI
Rangi ya ngozi yako ndio itakupa jibu ni nguo za rangi gani uvae kama ni rangi za kung’aa au kupoa na unaweza kujua kwa kufanya research ndogo mtandaoni au kuwauliza wataalamu wa mitindo au hata make-up artist
6)KUWA NA VIATU VYA AINA MBALIMBALI
Kuna wengine wanependa viatu vifupi au virefu basi kabati litajaa hivyohivyo tu hapana hauto kuwa stylish namna hio kwa maana kuna mavazi mengine yanahitaji viatu vya aina fulani tofauti na ulivyo navyo
5)TUPA/GAWA AU MODIFY NGUO UNAZO JUA ZIMEPITWA NA WAKATI
kuna watu huwa wana acha nguo hata kama imepitwa na wakati kwa matumaini ya fashion kujirudia kweli muda mwingine zinarudi na muda mwingine hazirudi ni bora utupe au ugawe ili kupata nafasi ya nguo zilizo kuwepo kwa wakati huo au uimodify iwe kiwakati uliopo
4)KUVAA ACCESSORIES NYINGI MUDA MWINGINE HAIKUFANYI UWE STYLISH
Huu mtindo uliingia sana mwaka ulio pita watu walikua wanavaa bangili nyingi mkononi au hereni au cheni muda mwingine unahitaji vitu vichache tu kama hereni,mkufu na kibangili cha kawaida
3)VAA NGUO ZINAZO ENDANA NA UMBO NA KUKUTOSHA
tafuta nguo zinazo kutosha na kuendana na mwili wako kuvaa nguo ambayo inakaribia kukutosha au haikutoshi kabisa haileti muonekano mzuri pia kuvaa nguo inayo bana sana tofauti na umbo lako. Vaa kitu kinacho endana na wewe
2)ANGALIA WATU WANAVAA NINI KATIKA KIPINDI HIKO
Tafuta magazeti ya fashion angalia ni kitu gani kipo kwenye trendy ikiendana na umri wako na umbo lako,hio itafkufanya uonekane unaenda na wakati
1) OMBA MSAADA KWA MTU WAKO WA KARIBU
Kama una rafiki au ndugu wa karibu ambae anajua maswala ya mitindo muombe msaada wa kwenda kununua nae mahitaji yako ya mavazi, ukiwa nae utapata ushauri kutoka kwake sio kama ukienda peke yako
Related posts
4 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Information to that Topic: afroswagga.com/dondoo/dondoo-7-za-kuwa-stylish/ […]
… [Trackback]
[…] Information on that Topic: afroswagga.com/dondoo/dondoo-7-za-kuwa-stylish/ […]
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/dondoo-7-za-kuwa-stylish/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/dondoo/dondoo-7-za-kuwa-stylish/ […]