SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Jinsi Ya Kuanza Kula Mlo Kamili Na Bora
Afya

Jinsi Ya Kuanza Kula Mlo Kamili Na Bora 

Kuanza kula mlo kamili ni bora ni kazi sana, wengi wetu tunashindwa kutokana na miundo ya Familia zetu tumezoa tukiamka asubuhi ni viporo,vitumbua nk, mchana ugali na usiku wali. Hii inatufanya tuishi kwa ajili ya kula na si kula kwa ajili ya kuishi.

Kama ungependa kuanza kula kwa ajili ya kula hizi ni njia chache za kukusaidia.

Anza kwa kuhesabu matokeo

 

 

– nini unapata kutokana na mlo unakula sasa? unapata matokeo chanya au hasi? wengi tunaichukia miili yetu kwa kuwa minene, vitambi na kuchukia baadhi ya maeneo ya miili yetu. Lakini haya si matokeo makubwa sana kuna yale ambayo si ya kuchekea kama

 • matatizo ya moyo
 • hatari ya kupata kansa
 • kunenepa kupita kiasi
 • kuanza kujichukia na mengineyo mengi.

Kisha fikiria faida za kula mlo kamili na bora 

 • kupunguza nafasi ya kupata magonjwa
 • kujiamini
 • kuwa productive
 • kuwa na nguvu na vingine vingi vizuri

Tafuta motisha 

 

 

 • jifunze faida za vyakula mbalimbali hii itakusaidia kujua kipi kinakufaa na kipi hapana
 • follow accounts zinazo elimisha kuhusu vyakula bora
 • anzisha urafiki na watu wenye lengo moja na wewe
 • jifunze kupika vyakula bora kisasa ili uweze kufurahia mlo wako

Anza taratibu

Kosa kubwa ambalo watu wengi wanalifanya ni kutaka kuanza kwa ukubwa na hii si kwenye chakula tu bali hata katika maisha yetu ya kawaida, huwezi kumuachisha mlevi pombe kwa ghafla atateseka anza kwa kupunguza milo fulani taratibu kama punguza kula sukari na chai na anza kunywa chai na sukari, punguza kula viporo au vitumbua badala yake tafuta mikate ya brown etc. kama umezoea kula unhealthy food kwa week nzima jaribu kupunguza ziwe ziku sita au tano taratibu mpaka utakapo zoea kabisa.

Gawanya – namna rahisi ya kuacha tabia mbaya ni kuzireplace na zile nzuri, replace unhealthy food na zile healthy food

 • Kunywa green tea badala ya coffee
 • maji na fresh juice badala ya soda
 • mchele wa kahawia badala ya mchele mweupe
 • mafuta ya nazi au olive badala ya yale processed ya kupikia.

Jifunze mapishi marahisi yenye kutumia muda mchache

jifunze mapishi rahisi ya mlo kamili hii itakusaidia kuepukana na kukununua vitu vya madukani au junky food, fanya hii iwe tabia yako. unaweza kutafuta siku mbili au tatu ukapika vyakula vingi na kuvihifadhi kwenye fridge ili pale usikiapo njaa unapasha na kula instead of ya kwenda kununua chips au burger

Remba sahani yako – vyakula hivi vinaweza visiwe na sura nzuri sana usoni mwako kwaio jambo jema ni kujaribu kukifanya kiwe kizuri kadri ya uwezo wako na utakavyo weza kula, ongeza taste unazo zipenda, weka vitu vya rangi rangi kama carrot, hoho za kijani, njano, nyekundu etc.

Rudia hizi tips mara kwa mara na utajikuta umezoa.

 

Related posts

1 Comment

 1. crumpets disposable vape https://exotichousedispensary.com/product/springfield-farm-carts/

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/dondoo/jinsi-ya-kuanza-kula-mlo-kamili-na-bora/ […]

Comments are closed.