SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

JINSI YA KUSAFISHA MIGUU
Dondoo

JINSI YA KUSAFISHA MIGUU 

Miguu ni sehemu ya mwili inayotumika sana inatumika katika kutembea na kufanya shughuli zako za kila siku. Hii inamaanisha miguu inabidi iangaliwe zaidi na ipewe care ya hali ya juu ili kuifanya iendelee kukubeba na kufanya shughuli zako za kila siku. Kujali na kuiangalia miguu yako itakusaidia sana kuepukana matatizo ya ngozi za miguu kama Athlete’s foot au aina nyingine ya fangasi . Wakati wote miguu yako inatakiwa iwe katika hali nzuri na ya kupendeza.

Vidokezo hivi vya kuangalia miguu yako vinafaa kwa wanawake na wanaume ukiacha sehemu ya kupaka rangi ya miguu kwa wanaume.

1.Hakikisha unaosha miguu yako kila siku kwa maji safi na sabuni.

Zweetvoeten
Katika kutimiza majukumu yako ya kila siku tunatembea sana toka sehemu moja kwenda nyingine, miguu inakuwa imepitia kwenye vumbi  na uchafu kibao pale siku inapoisha. Fanya zoezi la kuiosha miguu yako ni sehemu ya utaratibu wako wa kila siku kabla hujalala hata kama hutaoga usiku huo . Isafishe vizuri kwa sabuni huku ukizingatia zaidi sehemu za katikati ya vidole vyako. Futa miguu yako kwa taulo au kitambaa kisafi na kikavu kwa umakini zaidi ili unyevu wote uishe, usilale na miguu iliyo na unyevu ni mwanzo wa kuzalisha vijidudu vya kuleta harufu mbaya.
2. Ipe miguu yako treatment ya kusafishwa/ pedicure ikiwezekana kila baada ya wiki mbili

pedicures

Sio lazima kupaka rangi kucha kila unapofanya pedicure kama si mpenzi wa kupaka rangi, ila pedicures zinasaidia sana kufanya nyayo na vidole vyako viwe laini na nyororo huku ukiondokana na ngozi ngumu/magaga. Si lazima ifanyike saluni na upoteze hela, inaweza ikafanyika nyumbani kwako kwa kufuata hatua zifuatazo

  • Loweka miguu yako kwa dakika 5 – 10 katika beseni kubwa lenye maji uvuguvugu. Unaweza kuongeza matone ya mafuta kama olive oil au hata lotion uitumiayo mwilini ili kuongeza moisture na kufanya miguu ilainike zaidi. Unaweza ukailoweka kwa muda wowote uupendao kama utapenda zaidi kurelax na kuifanya ngozi yako ilainike zaidi.
 • pedicure
  • Sugua miguu yako kwa kutumia scrub ili kuondoa layer ngumu na iliyokufa ili ubaki na layer laini. Kusugua/exfoliate ngozi ngumu ya kisigino sugua kwa kutumia brush au jiwe maalumu la kusugulia hakikisha unasugua kwa utaratibu kiasi na si kwa nguvu sana ili kukupunguzia maumivu ndiyo ni ngozi ngumu lakini kama layer ngumu ikitoka inabaki delicate skin ambayo ni laini na nyororo!
 • Kata kucha zako katika shape uipendayo ila hakikisha si katika shape ya mduara ili kupunguza tatizo la kucha kuotea kwa ndani (ingrown toenails). Kama unapenda shape ya mduara waweza kuzikata katika shape ya kawaida na ukazipiga msasa/file kuzipa umbo ulipendalo. Hakikisha kucha unazikata katika urefu wa kawaida zisiwe fupi sana.
 • Kumbuka ngozi inayoizunguka kucha zako/cuticles waweza kupaka mafuta kiasi au lotion uipendayo ili kuzilainisha na zirudishe nyuma kiasi kwa kutumia kijiti maalumu cha kufanyia hivyo. Angalizo usirudishe sana ngozi hiyo nyuma unaweza ukaijeruhi na ni rahisi kupata maambukizo ya fangasi kama hilo likitokea. Kuna watu hawapendi kusogeza cuticles zao ni uamuzi sahihi tu.

3. Zingatia haya

 • Kama ni mpenzi wa rangi za kucha hakikisha umesafisha kucha zako kwa kutumia remover. Angalizo: Jitahidi kutumia acetone-free remover, sababu acetone inazifanya kucha kuwa kavu na ngozi inayoizunguka kuwa kavu pia.
 • Tumia toe-separators ili kutenganisha vidole vyako na kuepusha kupakaza rangi yako vidole vingine
 • Tumia base-coat hii inasaidia kuifanya rangi yako iwe smooth katika upakaji wake.
 • Paka rangi shade uipendayo na tumia ‘three-stroke method’ yaani paka mara moja kila upande wa kucha na malizia katikati ili rangi ipakwe kucha nzima. Paka coats mbili za rangi ili kuifanya idumu zaidi.
 • Baada ya dakika 10 tumia topcoat ya rangi ili kuifanya rangi idumu zaidi na ing’ae zaidi.

Moisturize moisturize miguu kila siku. Paka lotion au foot cream kama utaratibu wako wa kila siku. Njia rahisi ambayo hata mimi naitumia ni kupaka mafuta/vaseline kwenye miguu yangu kabla ya kuingia kitandani hii inagurantii kuifanya miguu asubuhi iwe laini na nyororo. Hakikisha usiache sehemu za kati za vidole vyako viwe vina unyevu hii inaweza ikakuletea fungus na magonjwa mengine ya ngozi.

Related posts

4 Comments

 1. helpful site

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/dondoo/jinsi-ya-kusafisha-miguu/ […]

 2. cane corso puppies

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/dondoo/jinsi-ya-kusafisha-miguu/ […]

 3. Oregon shroom dispensary

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/dondoo/jinsi-ya-kusafisha-miguu/ […]

 4. Magic mushroom capsule

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/dondoo/jinsi-ya-kusafisha-miguu/ […]

Leave a Reply