SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Namna Ya Kuboresha Afya Yako Wakati Huu Wa Isolation
Afya

Namna Ya Kuboresha Afya Yako Wakati Huu Wa Isolation 

Kama ambavyo sote tunajua tumeambiwa tuepuke misongamano, kuna wale ambao wameambiwa wafanyie kazi nyumbani, kuna wale ambao wanaenda kazini lakini wana practice social distance etc.

Hii inapelekea wengi wetu kuwa nyumbani na kuwa karibu na vyakula, lakini pia kufungwa kwa sehemu za mazoezi ( gym ). Kuna aina mbili za watu watakao toka kwenye isolation, ambao watatoka wamenenepa na wale ambao watatoka na body goals chagua moja.

Leo tunakuletea namna ambavyo unaweza kurekebisha afya yako wakati tupo katika Isolation

  • Kufanya mazoezi hakuhitaji gym

Kuna application mbalimbali za mazoezi ambazo unaweza kutumia kufanya baadhi ya mazoezi madogo madogo nyumbani, tenga muda wako kati ya asubuhi au jioni na ufanye mazoezi husika mfano: Kutembea tembea katika uwanja wa nyumba yako, Kuruka kamba, Squats hazihitaji kwenda gym lakini pia ni nzuri katika ku-improve immune zako na kutoka jasho ambapo ni moja ya vitu tunashauriwa kufanya ili kuepuka maambukizi ya Covid19

  • Epuka Kula Un-Healthy Food

Wakati huu wengi wetu tunatumia kujisosomola kwa kula vyakula ambavyo si vizuri na afya zetu, badala yake chagua vyakula ambavyo vinafaa lakini pika vizuri. Mfano: Badala ya kunywa soda, tengeneza juice yako nyumbani. Instead ya kula chips za kukaanga na kuku, pika mchemsho wako vizuri, Badala ya kula biscuits na chocolate anza kula matunda kama apples au machungwa,

  • Kunywa Vimiminika

Hapa hatumaanishi unywe soda au processed juice, hapa tunamaniisha kunywa juice ambazo ni fresh au muhimu zaidi ni kunywa maji. Maji sio tu yanasaidia katika ngozi yako lakini pia huwa yanaondoa uchovu. Lakini pia unaweza kuongezea vitu kama limao, tango, tangawizi ili kuinua immune system zako.

  • Lala Vyema

Ikiwa unafanyia kazi nyumbani huitaji kuamka asubuhi subuhi kujiandaaa au hata kama unaamka asubuhi basi hakikisha una tenga masaa machache mchana kujipumzisha, kupata usingizi mchache kuna madhara mentally, physically na hata katika Immune system zetu. Hii haitasaidia tu katika kuepukana na COVID 19 bali pia katika kupumzisha mwili, akili na kufanya ngozi zetu ziwe bora

Well Afromates Stay Safe, Safisha Mikono Yako Kwa Maji Tiririka, Vaa Barakoa Unapokuwa Katika Misongamano, Practise Social Distancing Na Kuwa Healthy.

Related posts

1 Comment

  1. minermaster

    … [Trackback]

    […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/dondoo/namna-ya-kuboresha-afya-yako-wakati-huu-wa-isolation/ […]

Comments are closed.